TAARIFA KUHUSU HALI YA UJENZI WA JENGO LA OFISI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA
Posted on 15 November 2022HALI YA MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA OFISI YA MKURUGENZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA.
Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ilipokea shilingi 1,000,000,000.00 katika bajeti ya mwaka 2021/2020 fedha kutoka serikali kuu kwa ajili ya kujenga jengo la ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Utekelezaji wa Mradi huu ułitakiwa kuanza mwaka wa fedha 2021/2022 lakini ujenzi haukuweza kuanza kwa wakati.
Changamoto kubwa ya kuchelewa kuanza kwa Mradi huu ni Mgogoro wa Kisiasa wa Eneo la ujenzi uliochukuwa takribani miezi kumi na tano (15) na hatimae ujenzi huo ukaamuliwa ukafanyike katika Kata ya Mahembe.
Hivyo kazi ya ujenzi huu ikaanza kutekelezwa na Mkandarasi mnamo Tarehe 16/08/2022.
Kumekua na changamoto nyingine mbalimbali katika utekelezaji wa mradi sababu ya ufinyu wa wazabuni inayopelekea uhaba katika upatikanaji wa vifaa Mfano. Nondo, Saruji na Kokoto kwani kuna Klasha moja tu linalotengeneza Kokoto zinazofaa nakuhitajika kwa ujenzi wa ghorofa ambalo liliharibika kwa takribani mwezi mmoja.
Saruji pia ziliadimika Mkoa mzima wa Kigoma kwa muda wa mwezi moja.
Uhaba wa watumishi katika Kitengo cha Manunuzi, ambapo Kitengo cha Manunuzi hakikuwa na Mkuu wa Kitengo mzoefu kwa muda wa miezi mitano (5) na Kitengo hiki kuwa na watumishi wawili kwa kipindi chote na hivyo kupelekea Kitengo kuelemewa na kazi kuzingatia kwamba Halmashauri ina miradi mingi inayotekeleza.
UTATUZI WA CHANGAMOTO
Halmashauri imeendelea kuomba kuletewa watumishi ili kutatua tatizo la watumishi na tunashukuru tayari tumeshapokea Mkuu wa Kitengo cha Kitengo cha Manunuzi.
Halmashauri kununua baadhi ya vifaa vya ujenzi kiwandani mf. Nondo na Mabati.
Kwa sasa changamoto zimetatuliwa na ujenzi wa Mradi unaendelea kwa kasi, ujenzi huo kwa awamu ya kwanza unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Disemba 2022.
Kiujumla miradi yote ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Inaendelea vizuri na hakuna Mradi ambao umesimama kama inavyosemekana. Ipo miradi ambayo imekamilika na kutoa huduma na ipo mingine ambayo ujenzi bado unaendelea.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA
15 NOVEMBA 2022