ZIARA YA MKUU WA MKOA WA KIGOMA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA

Tarehe 13 April 2022 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mh. Thobias Andengenye amefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma. Ziara hiyo imehusisha kufuatilia na kuhamasisha zoezi la uwekaji wa Anwani za Makazi pamoja na kukagua miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Katika zoezi la uwekaji wa Anwani za Makazi, Mkuu wa Mkoa amesisitiza kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yaliyowekwa katika Wilaya, Mkoa na Taifa. Mkuu wa Mkoa pia amewahamasisha wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kutoa ushirikiano kwa makarani wanaopita katika makazi ya watu kuchukua data za Anwani za Makazi. Pia Mkuu wa Mkoa amewaomba wananchi kuwa walinzi wa vibao vya Anwani za Makazi ili kuhakikisha hakuna uhalibifu wa miundombinu hiyo.
Pichani juu: Mkuu wa Mkoa Mh. Thobias Andengenye (Mwenye Suti Nyeusi) akiongea na wananchi katika Kata ya Mwandiga, Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Pichani juu: Kibao kikionesha uwelekeo wa barabara ya Kiwanjani katika Kata ya Mwandiga, Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Mkuu wa Mkoa pia amefanya ukaguzi wa mradi wa matundu 12 ya vyoo katika shule ya msingi Nkema iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma. Mkuu wa Mkoa amesisitisha kuwekwa kwa miundombinu ya Maji haraka ili vyoo hivyo vianze kutumika.
Pichani juu: Mkuu wa Mkoa Mh. Thobias Andengenye (Wa Pili mwenye Suti Nyeusi) akipokea taarifa ujenzi wa matundu 12 ya vyoo katika shule ya msingi Nkema iliyopo Kata ya Mwandiga kutoka kwa mwalimu Mkuu (Wa kwanza kushoto). Wengine ni viongozi wa Wilaya ya Kigoma.
Pichani juu: Mkuu wa Mkoa Mh. Thobias Andengenye (Mwenye Suti Nyeusi) akikagua vyoo katika shule ya msingi Nkema.
Pichani juu: Majengo mawili ya vyoo yenye matundu 12 katika shule ya msingi Nkema.
Picha ya pamoja ya Mkuu wa Mkoa Mh. Thobias Andengenye (Katikati mwenye Suti Nyeusi) na watumishi walimu wa shule ya msingi Nkema iliyopo Kata ya Mwandiga pamoja na viongozi wa Wilaya ya Kigoma wakati wa ziara yake tarehe 13 Aprili 2022.
Mkuu Mkoa Mh. Thobias Andengenye amemalizia ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwa kukagua ujenzi wa nyumba ya watumishi katika Zahanati ya Kidahwe. Mkuu wa Mkoa amesisitiza kumalizika haraka kwa mradi huo ili watumishi hao wa afya waweze kuishi karibu na kituo cha kutolea huduma
Pichani juu: Mkuu wa Mkoa Mh. Thobias Andengenye (Mwenye Suti Nyeusi), Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Lusajo Mwakajoka (Wa kwanza kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bw. Nassir Kirusha (Wa pili kutoka kulia), wakikagua ujenzi wa nyumba ya watumishi katika Zahanati ya Kidahwe.
Pichani juu: Jengo la nyumba ya watumishi katika Zahanati ya Kidahwe ikiwa hatua ya Linta.