WALENGWA WA KAYA MASKINI WAHIMIZWA KUENDELEZA UJUZI NA MIRADI WALIYOANZISHA

Walengwa wa mfuko wa kunusuru Kaya maskini TASAF wamehimizwa kuendeleza ujuzi na miradi waliyoanzisha ili kuimarisha na kuboresha maisha ya kaya baada ya mpango wa pili kuhitimishwa ili kuruhusu mpango mwingine kuanza.
Mwito huo umetolewa na Mratibu wa TASAF wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Jummane Duguda leo tarehe 20 Agosti,2025 wakati akizungumza na Maafisa wanaokwenda kutekeleza zoezi la uhawilishaji fedha kwa walengwa kwenye maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Walengwa wa Kaya maskini wamehimizwa kufanya hivyo kwa kuwa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN II) unaotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF, pamoja na wadau wa maendeleo, unatarajiwa kuhitimishwa rasmi mwezi Septemba 2025 kabla ya kuanza kwa mpango mwingine.
Ameongeza kuwa Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo jamii - TASAF imeleta mabadiliko chanya kwa kaya maskini za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kupitia uhawilishaji wa fedha kwa walengwa, ajira za muda, vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana, pamoja na ujasiriamali.
Serikali kupitia Mpango wa Kunusuru
Kaya Maskini imeweza kuboresha huduma ya afya, elimu, kipato na ujuzi wa kaya maskini zaidi ya milioni 1.37. 4 kwa nchi nzima huku Mpango ujao wa TASAF wa kuhudumia Walengwa ukiwa katika hatua za mwisho za maandalizi ambapo Kaya za mpango ujao zitatambuliwa upya.