ZAIDI YA TSH 60,000,000/= ZIMETENGWA KWA AJILI YA KUIMARISHA LISHE
Posted on: February 7th, 2024By mwifyusil@
Halmashauri ya wilaya ya Kigoma imetenga fedha 60,062,500/= kwa ajili ya kuimarisha utoaji wa lishe katika Halmashauri ya Kigoma.
Akiongea Mratibu wa lishe, Ndugu James Swai katika kikao cha kamati ya lishe ya Halmashauri ya wilaya kilichofanyika leo tarehe 07, februari, 2024, Amesema tumejipanga vizuri kuhakikisha hilo Halmashauri ya wilaya ilipanga kutoa Tsh 5,005,208.33, kila mwezi ili kufikia malengo ya kutoa kiasi cha Tsh 60,062,500/= kwa mwaka ili kupunguza tatizo la udumavu na utapiamlo.
Aidha amesema katika robo ya kwanza ya mwaka kamati ya lishe wilaya imetekeleza shughuli mbalimbali za lishe ikiwa ni Pamoja na utoaji wa ushauri wa lishe kwa jamii katika vijiji zaidi ya 41, Utoaji wa dawa za kuongeza wekundu wa damu(feFO) kwa wanawake waja wazito,kuazimisha siku ya saliki duniani kwa vijiji 41, Kuazimisha siku ya mayai duniani katika kata ya bitale na kugawa mayai zaidi ya 700’ kubaini Watoto wenye udumavu kwa kupima Watoto 23756.
Hata hivyo mratibu amesistiza kuhakikisha kila shule inatoa chakula shuleni, aziwataka idara zote zishirikiane kushawishi wazazi kuchangia chakula shuleni.
Mafisa lishe wakiwa na CC katikati wakifuatilia kikao cha Lishe.
Wadau na wataalamu wakifuatilia kikao cha Lishe