WANANCHI WALIOATHIRIWA NA MTITIO WA ARDHI KATA YA NYARUBANDA WATAKIWA KUACHA KUFANYA SHUGHULI ZA KIBINADAMU KATIKA MAENEO HAYO
Posted on: April 12th, 2024Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kigoma Jabiri Timbako amewataka wananchi wa kijiji cha Nyarubanda, kata ya Nyarubanda kuhama katika eneo lililoathirika na mpasuko wa ardhi uliosababisha baadhi ya nyumba kupasuka.
picha za nyumba zilizoathirika na mtitio wa ardhi
Mpasuko huo wa ardhi uliotokea jana umeathiri eneo lenye ukubwa wa zaidi ya kilometa 20 uliosababisha uharibifu wa nyumba nne zenye takribani watu 20 sambamba na mashamba yao.
Kaimu Mkurugenzi ameyasema hayo alipotembelea maeneo yaliyoathiriwa akiambatana na mkuu wa wilaya hiyo pamoja na viongozi wengine wa kamati ya ulinzi na usalama.
“Nataka wananchi waondoke mara moja katika maeneo haya kwani sio salama tena kwa shughuli za kibinadamu” Amesema Timbako.
Naye mkuu wa wilaya ya Kigoma Salum Kalli amesema serikali inashughulikia changamoto hiyo iliyojitokeza ili kuhakikisha wahanga wanawezeshwa ili waweza kukidhi mahitaji yao ya kila siku ikiwa ni pamoja na kutafuta makazi ya muda kutoka kwa majirani zao.
Mkuu wa wilaya akizungumza na wananchi wa eneo liloathiriwa na mtitio wa ardhi
Amesema kamati ya maafa tayari imeanza kuchukua hatua kwa kufanya tathimini ya uharibifu katika maeneo hayo kwa hatua zaidi na kuwataka wananchi kuzingatia maelezo ya watalamu ya kuacha mara moja kufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo hayo ili kuepuka madhara zaidi kwani mpasuko bado unaendelea