VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA H/W KIGOMA WAPIGWA MSASA NA OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUHUSU SHERIA,HAKI NA WAJIBU
Posted on: October 4th, 2024Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Viongozi wa vyama vya Siasa wameaswa kuzingatia Sheria za nchi na Sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa ili kuendelea kudumisha Amani,Uzalendo na umoja wa Kitaifa uliopo nchini.
Wito huo umetolewa leo tarehe 22 Oktoba,2024 na Afisa kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa Bw.Nelson Hutty wakati wa Mafunzo kuhusu Sheria,Haki na wajibu wa vyama vya Siasa kwa Viongozi wa vyama mbalimbali vya Siasa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwa lengo la kuwapatia elimu na Uelewa wa mambo mbalimbali kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Bw.Hutty ameeleza kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inalenga kuwapa elimu Viongozi wa Siasa ili kuhamasisha Ushiriki wa vyama kwenye Uchaguzi,uhusiano mzuri na wadau wengine, uvumilivu wa Kisiasa na Utii wa Sheria bila shuruti kwaajili ya mustakabali wa umoja na Muungano wa Taifa la Tanzania.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya Viongozi wa vyama vya Siasa wamesema wanaishukuru Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa kuamua kuwaletea Mafunzo hayo,kwakuwa yanawakumbusha Haki na wajibu wao na kuwawezesha kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na chaguzi nyingine kwa kuzingatia Sheria na taratibu za nchi.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,unatarajiwa kufanyika tarehe 27, Novemba 2024