VIJANA ZAIDI YA 539 WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA KUNUFAIKA NA MRADI WA CASHPLUS
Posted on: February 7th, 2024Mfuko wa maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Kigoma (TASAF) kwa Udhamini wa UNICEF, Umendesha mafunzo ya ujana salama(CASHPLUS)
Mafunzo haya yametolewa kwa vijana wa kike na wakiume wenye umri kwanzia miaka 14-19, wale waliyohitimu darasa la saba , form four na hawakuendelea na masomo Pamoja na walioacha shule na ambao hawakuenda shule kabsa , vijana wote wanaotoka katika familia za kaya masikini wanufaika na mfuko wa TASAF.
Mafunzo haya yanalenga kuwajengea vijana uwezo wa kujiendeleza kimaisha na ujenzi wa stadi za Ujasilimali zinazohusiana na uandaaji wa mipango ya biashara na uzalishaji wa rasilimali fedha,kijamii na kijinsia pia mafunzo haya yameambatana na utoaji wa elimu ya afya ya uzazi na jinsia
Mafunzo haya yatakomboa vijana kutoka kaya masikini kujikwamua na mnyororo wa umasikini na kusaidia vizazi vijavyo kwenye adha ya umasikini.
Aidha baada ya mafunzo haya kila kijana aliyepata mafunzo haya atapewa mtaji wa biashara kulingana na mpango wa biashara aliuandaa .
Vijarunga wakiwa darasani wakipatiwa mafunzo katika vijiji vyao
Mentor akizungumza na vijarunga
Mafunzo yanaendelea