UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA

Serikali imejenga mabweni 2 katika Shule ya Sekondari Kaseke iliyopo Kata ya Simbo kwa thamani ya shilingi milioni 58 ili kuwaondolea Wanafunzi adha kusafiri mwendo mrefu kufuata huduma ya Elimu.
Mabweni haya yamewawezesha Wanafunzi kuwa na utulivu na kupata muda mzuri wa kujisomea na hatimaye kufanya vizuri kwenye masomo yao na kufaulu mitihani.
Huu ni mwendelezo wa uboreshaji wa Miundombinu katika Sekta ya Elimu kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma unaofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hususan katika kipindi hiki cha Uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.