D.C DKT.CHUACHUA APOKEA MADAWATI 100 KUTOKA KAMPUNI YA SAVONOR TANZANIA

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mhe.Dkt.Rashid Chuachua amewataka wadau kuendelea kuiunga mkono Serikali katika jitihada za kuboresha miundombinu kwenye shule za msingi na Sekondari ikiwemo madawati.
Dkt.Chuachua ametoa rai hiyo leo tarehe 04, Agosti,2025 wakati wa hafla ya kukabidhiwa Madawati 100 kutoka kwenye Kampuni ya Savonor Tanzania yatakayopelekwa kwenye shule za msingi za Nyangova,Bubango,Chankabwimba na Sokoine katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Dkt.Chuachua ameishukuru Kampuni ya Savonor Tanzania kwa msaada wa madawati na kuwaasa wasichoke kuendelea kutoa madawati kwasababu bado kuna uhitaji hasa kwa shule za msingi.
Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ina jumla ya shule za msingi za Serikali 109 huku ikiwa na Wanafunzi 64,053 ambapo kwa sasa upungufu wa madawati ni 11,054 ili kuendana na uwiano wa kitaifa wa dawati moja kwa wanafunzi 3.