STENDI YA MWANDIGA KUANZA KESHO

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kigoma Jabil Timbako amesema makubaliano waliyofanya na chama cha usafirishaji wa abiria Kigoma (KIBOA) juu ma maboresho ya stand ya Mwandiga yamekalika na ipo tayari kuanza kazi kuanzia kesho tarehe 12 Machi 2024.
“Siku za nyuma, miundombinu ya stand iliharibika,wafanyabiashara wa magari wakagoma kuingiza magari stand,tulikaa na kuzungumza nao,wakatuelekeza mambo ya kufanya ili waweze kuingiza magari tena stand, na sisi kama halmashauri tumefanyia kazi majukumu yote tuliyoambiwa kutekeleza na sasa tupo tayari kuendelea na kazi” Amesema Timbako
Amesema miongoni mwa maboresho waliyokubalina na yamekamilika ni pamoja kuweka kifusi na kusawazisha sehemu ya kuegesha magari ili kuepusha uharibifu, kujenga miundombinu ya choo, kujenga kibanda cha kupumzikia abiria pamoja na kujenga fensi ambavyo vyote vimekamilika.
Amesema katika eneo hilo lipo eneo la wachuuzi wadogo kwaajili ya kujenga vibanda vya biashara zao na kwamba ili kuondoa uchafuzi wa mazingira litawekwa eneo maalumu kwaajii ya kutupa taka.
“Tumefanikiwa kuongeza urefu na upana wa stand ili kuhakikisha magari ya yanapata sehemu ya ya kutosha, na wafanyabiashara wanafanya biashara zao kwa uhuru, tumeongwza urefu kutoka mita 90-105 na upana kutoka mita 50-60,na tutaendelea kuongeza ukubwa kulingana na uhitaji” Amesema Mkurugenzi
Hata hivyo amesema maboresho mengine yanaendelea kufanyika huku stand ikiendelea kufanya kazi ili kuingiza kipato,ikiwemo marekebisho ya kuweka miundombinu ya maji kutoka mamlaka za maji, kwani kwa sasa maji yatakayotimika yatahifadhiwa kwenye tenki na ndio, na yatachotwa kutoka mto na mabomba yaliyoka karibu pamoja na taa kwaajili ya ulinzi ambayo yote yatakamilika ndani ya wiki moja.
Wakizungumza kwa niaba ya wananchi Semeni Jumanne, mkazi wa tarafa ya Mwandiga amesema kukamilika kwa stendi hiyo kutaepusha ajali barabarani na kuiomba halmashauri kuweka miundombinu ya maji ya uhakika chooni ili kuepusha watu kubeba maji kwani yanapatikana ndani ya umbali mrefu takribani kilomita tano.
Naye Shaban Salum amesema ili kuepusha wizi wa mali za abiria wanaosafiri muda huo au watakaolala stendi kwaajili ya kuanza safari kesho yake, anaomba taa zitakaziwekwa ziwake kwa nyakati zote za usiku.
Kwa upande wake katibu wa KIBOA, Almasi Juma amesema kwa marekebisho yaliyofanyika wapo tayari kuamua stendi na kwamba atafanya uhamasishaji wa madereva wote kuingia humo na asiwepo yeyote atakaye kiuka taratibu na kuiomba halmashauri kukamilisha miundombinu iliyosalia ndani ya muda waliojipangia