SERIKALI KUENDELEA KUSIMAMIA MPANGO WA KUHIFADHI MAZINGIRA KWA AJILI YA USALAMA WA MAZINGIRA KWA KIZAZI CHA SASA NA CHA BAADAE
Posted on: September 15th, 2024Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Godfrey Mnzava amesema Serikali itaendelea kusimamia Sera na mipango ya uhifadhi wa Mazingira kwa ajili ya usalama wa Mazingira kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Mnzava ametoa kauli hiyo alipotembelea na kukagua eneo la uhifadhi wa Mazingira katika Shule ya Sekondari ya kutwa Msimba iliyopo Halmashauri ya Kigoma.
Amesema kunachangamoto ya uharibifu wa Mazingira kutokana na matumizi makubwa ya miti kwa ajili ya nishati ya kupikia.
Amesema Taaisi za Umma na watu binafsi wanapaswa kujikita katika matumizi ya Nishati safi ili kuepuka uharibifu mkubwa wa Mazingira.
Katika hatua nyingine kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge ameitaka jamii kuepuka ukatili wa kijinsia ikiwamo manyanyaso dhidi ya wanawake na watoto unaopelekea ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
Jamii imejenga utaratibu wa kumaliza matatizo yao kifamilia hali inayosababisha wakosefu kuendelea kutekeleza vite do vya kikatili, hivyo pale inapobainika vitendo hivyo jamii ijenge utaratibu wa kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama.
Amesema baadhi ya watu baada ya kutendewa vitendo vya ukatili wa kijinsia hukaa kimya, jambo linalosababisha vitendo hivyo kuwa endelevu na vyenye kuendelea kuleta madhara kwa jamii.
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Kigoma umezindua mradi wa Maji Kidahwe, umezindua vyumba vinne vya madarasa katika Shule ya Msingi Kidahwe, uzituzi wa kotuo cha mafuta, kutembelea mradi wa uhifadhi wa Mazingira Shule ya Sekondari Msimba, umezindua daraja la mawe Mgaraganza-Bweru sambamba na kutembelea Klabu za wapinga rushwa katika Shule ya Sekondari Mwandiga.