RAS RUGWA AAGIZA HOSPITALI YA WILAYA YA KIGOMA KUANZA KUTOA HUDUMA
Posted on: May 23rd, 2024Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Ndg. Hassan Rugwa amemwagiza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kuhakikisha anasimamia ukamilishaji na uwekaji wa umeme na maji katika majengo ya Wodi za Hospitali ya wilaya ya Kigoma iliyopo Kata ya Mahembe katika Halmashauri hiyo.
Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya kigoma Aswile mwambembe akinukuu maelekezo ya RAS
Katibu tawala amesema Serikali ya awamu ya sita imetumia Fedha nyingi kujenga Hospitali hiyo, Ili iweze kutoa huduma kwa wananchi na kuwaondolea adha ya kwenda kufuata huduma za kibingwa katika Hospitali za mbali, amesema kwa kiasi kikubwa majengo yote ya msingi yamekamilika na vifaa vya kisasa tayari vipo, hivyo haoni sababu za Hospitali hiyo kutoanza kutoa huduma za matibabu kwa Wagonjwa wa nje na ndani amemtaka Mkurugenzi huyo kuhakikisha Hospitali hiyo inatoa huduma mara moja.
Sambamba na hilo Katibu Tawala , amesema agizo hilo linapaswa kwenda sambamba na ukamilishwaji wa miundombinu mingine inayoendelea kujengwa katika Halmashauri ya Wilaya hiyo, Huku akisisitiza zaidi juu ya ukamilishaji wa jengo la Utawala linalojegwa katika Kata ya Mahembe na kusisitiza kuwa tarehe ya kuhamia jengo hilo ni ileile.
picha kuonyesha hatua za ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri ya wilaya ya kigoma kata ya mahembe
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ndg. Jabil Timbako amesema amepokea maelekezo hayo na kwa kushirikiana na Mkurugenzi pamoja na watumishi wengine watasimamia utekelezaji wa maelekezo hayo kikamilifu.
Ikumbukwe awali aliyekuwa Katibu tawala wa mkoa wa kigoma Ndugu. Albert Msovela aliagiza ifikapo tarehe 1 julai 2024, watumishi wote kuhamia katika jengo la utawala la mahembe liwe limekamilika au halijakamilika.
RAS kigoma akitotoa maelekezo kwa kaimu mkurugenzi Jabil Timbako na Eng. Paul nkuba akiwa katika jengo la utawala mahembe.
Jengo la utawala la mahembe lipo katika hatua za mwisho kabisa za ukamilishwaji mafundi wanapambana usiku na mchana kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo, kwa wakati ili watumishi waweze kuhamia kwa muda mwafaka.