MWENYEKITI WA HALMASHAURI NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WAMPONGEZA MKURUGENZI CHIRIKU KWA UTENDAJI WAKE
Posted on: September 2nd, 2024Mwenyeki wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Mhe. Joseph Nyambwe amemsifu na kumpongeza Chiriku Hamisi Chilumba, mkurugenzi wa Halmashauri ya Kigoma kutokana na utekelezaji bora wa majukumu yake.
Pongezi hizo amezitoa akihitimisha kikao cha robo ya nne cha baraza la madiwani kilichofanyika Agosti 30, 2024.
Mwenyekiti Nyambwe amesema "Tangu nilipokuwa mwenyekiti wa Halmashauri hii, Mkurugenzi wetu Chiriku amekuwa kiongozi Bora na wakipekee sana,
katika Kipindi kifupi alichokaa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, ameleta Mabadiliko Makubwa sana ya kiutendaji katika Halmashauri ,
Miradi iliyokuwa Ikisusua katika Kipindi Cha Chiriku Maendeleo ya Ujenzi yanaendelea kwa kiasi sana"
Vilevile amesema kuwa, Mkurugenzi Chiriku Chilumba amefanikiwa kurejesha amani kwa wafanyakazi, madiwani na wananchi wote kwa ujumla hali iliyopelekea ongezeko la ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Chiriku amekuwa Mshirikishaji na muwazi sana kwa kila Pesa ya miradi inapoingia, haya mambo huko nyuma hayakuwepo kabisaa . Ninamshukuru sana Rais wetu Dr. Samia Suluhu Hassani kwa kutuletea Chiriku".
Kwa upande wa viongozi wa vyama vya Siasa waliohudhuria katika baraza hilo,Shabani Kasugulu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) amekiri jitihada za Mkurugenzi huyo na kwamba ni kiongozi msikivu na anayesimama kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
Naye katibu wa Chama Cha Mapinduzi Rashidi Semendu amesema Chiriku Chilumba ni kiongozi wa kuigwa kutokana na utendaji kazi wake mzuri na kuwataka watendaji kuunga mkono jitihada zake kwa kutekeleza majukumu wanayopewa kwa mujibu wa kanuni na taratibu za kiutumishi.