MTITIO WA ARDHI WAZUA HOFU KUBWA KWA WANANCHI WA KATA YA NYARUBANDA WILAYANI KIGOMA
Posted on: April 12th, 2024Wananchi wa Kijiji cha nyarubanda kata ya nyarubanda iliyoko halmashauri ya wilaya ya Kigoma, wamejikuta wakiwa kwenye hofu na mashaka makubwa, baada ya kipande cha ardhi kinachokadiliwa, kuwa na ukubwa wa zaidi ya kilometa 20 kutitia na kusababisha mpasuko Mkubwa katika ardhi, ambao umepelekea uharibifu wa makazi na mashamba ya wananchi hao, hali hiyo imezua hofu kwa wananchi hao kwani mpaka sasa kaya kadhaa zimekosa makazi na mashamba yao yameathiliwa na mpasuko huo.
Picha kuonyesha mpasuko uliyosababishwa na mtitio wa ardhi nyarubanda
Picha kuonyesha makazi ya wananchi waliothiliwa na mtitio wa ardhi.
Hata hivyo tukio hilo limewashitua viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kigoma wakiongozwa na mkurugenzi wa halmashauri ya Kigoma Ndg. Chiriku Hamisi Chilumba, wamefika na kuyatembelea maeneo yalioathiriwa na tukio hilo na kuwataka wananchi waondoke mara moja katika maeneo hayo , kwani sio salama tena kwa shughuli za kibinadamu.
Naye mkuu wa wilaya ya Kigoma Mh. Salum Kalli akiongozana na kamati ya usalama ya wilaya ya Kigoma, amefika na kutembelea maeneo hayo na kuwataka wananchi wasiwe na hofu kwani serikali ipo na inalifuatilia kwa ukaribu tukio hilo na kuwahakikishia wahanga wa tukio hilo watawezeshwa ili kuweza kukizi mahitaji yao ya kila siku ikiwa ni Pamoja na kuwatafutia makazi ya muda kutoka kwa majirani zao.
Mkuu wa wilaya ya Kigoma Salum Kalli akiwa katika eneo la Kijiji cha nyarubanda lililoathiliwa na mtitio wa arthi.
Pia Mkuu wa wilaya amesema kamati ya maafa tayari imeanza kuchukua hatua kwa kufanya tathimini ya uharibifu katika maeneo hao kwa hatua zaidi na kuwataka wananchi kuzingatia maelezo ya watalamu ya kuacha mara moja kufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo hayo kwani mpaka sasa hali sii shwali kwani mpasuko bado unaendelea.
Naye diwani wa kata ya nyarubanda Gabriel chobariko amewashukuru viongozi wa halmashauri Pamoja na mkuu wa wilaya kwa kufika katika maeneo hayo amesema “tunamshukuru mweshimiwa Rais Samia Suruhu Hassani kwa kutuletea viongozi hawa, imekuwa kama zawadi kwetu ,nimekuwa diwani kwa miaka nane, lakini sijawahi kuona viongozi kama hawa, kwani wamekuwa sehemu ya jamii , kipaombele chao ni kutatua kero za wananchi , Mkuu wa wilaya anamwaka mmoja tu lakini ametembela kata hii mara tano na kutatua kero zetu,mkurugenzi ana miezi mitatu tu, lakini amekuwa msitari wa mbele kutatua kero zetu na jana asubuhi na mapema baada ya kusikia hili alifika na kamati yake, Mungu awabariki ”.