MKUU WA WILAYA YA KIGOMA AFANYA ZIARA KATIKA KATA YA KAGUNGA
Posted on: May 7th, 2023Na Mwandishi Wetu:
Tarehe 6 Mei, 2023 Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Salum Kalli alifanya ziara katika Kata ya Kagunga iliyopo Wilaya ya Kigoma, Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma. Mkuu wa Wilaya aliambatana na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Kigoma na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali, wakiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kagunga Mh. Joseph Nyambwe na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bw. Jabir Timbako. Pia Mkuu wa Wilaya ya Kigoma aliambatana na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na wataalamu kutoka Taasisi zilizopo katika Wilaya ya Kigoma.
Picha juu: Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiwa kwenye ziara.
Lengo la ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma ilikuwa ni kukagua Miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Kata ya Kagunga. Pia Mkuu wa Wilaya ya Kigoma alikwenda kwa lengo la kuongea na wananchi wanaoishi katika Kata hiyo ya Kagunga na kutatua changamoto za wananchi. Kata ya Kagunga ina vijiji viwili ambavyo ni Kijiji cha Kagunga na Kijiji cha Zashe. Kata hiyo inapatikana Mwambao wa Ziwa Tanganyika na pia inapakana na Nchi ya jirani ya Burundi.
Pichani juu: Timu iliyoambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma
wakiangalia maendeleo ya ujenzi wa Soko la Kagunga.
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma na viongozi walioambatana nao wametembea Miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Kata hiyo ambayo ni Soko la Kimkakati la Ujirani mwema, Kituo cha Afya Mwamgongo pamoja na barabara inayounganisha Bandari ya Kagunga na nchi jirani ya Burundi.
Pichani juu: Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Salum Kalli na viongozi wengine wakikagua
maendeleo ya barabara inayounganisha Bandari ya Kagunga na nchi jirani ya Burundi.
Kupitia kikao cha ndani na baadae kufuatiwa na mkutano wa nje na wananchi, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma aliongea na wananchi na kutatua changamoto zao hapo hapo huku zingine zikiendelea kutatuliwa. Miongoni mwa changamoto zilizoibuka ni pamoja na vitambulisho wa utaifa, upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa, mfumo mzuri wa matumizi ya Maji yanayosambazwa na RUWASA pamoja na upatikanaji wa umeme. Pia Mkuu wa Wilaya ya Kigoma amewaomba wananchi wa Kata ya Kagunga kudumisha amani tuliyonayo.
Pichani juu: Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Salum Kalli
akiongea na viongozi wa Kata na vijiji katika kikao cha ndani.
Pichani juu: Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Salum Kalli
akiongea na viongozi wa Kata na vijiji katika kikao cha ndani
Pichani juu: Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigoma ikiwa katika
kikao cha ndani cha viongozi wa Kata ya Kagunga na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma.
Pichani juu: Viongozi wa Kata na vijiji vya Kagunga na Zashe
wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kigoma katika kikao cha ndani.
Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ndg. Rashid Semindu amesisitiza kwamba wao wanaendelea kusimamia ilani kuhakikisha inatekelezwa.
Pichnai juu: Wananchi wa Kata ya Kagunga wakimsikikiza
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Salum Kalli
Huku Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma amewahakikishia wananchi na viongozi kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha miradi iliyoanzishwa inamalizika kwa wakati, na kwamba wataendela kutoa huduma kwa wananchi.
Pichani juu: Wananchi wa Kata ya Kagunga wakiwa
katika mkutano wa nje na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma.