MKUU WA WILAYA AITAKA JAMII KUTAMBUA FURSA ZA KIMAENDELEO KWA WANAWAKE
Posted on: March 1st, 2024Mkuu wa wilaya ya Kigoma, Salum Kalli amewataka wadau wa masuala ya kijinsia kushirikiana na halmashauri kutoa elimu kwa jamii ili kujenga uelewa kuhusu changamoto zinazokwamisha maendeleo ya wanawake na usawa wa kijinsia.
Amesema ni muhimu jamii ikatambua fursa zilizopo za kimaendeleo zitakazomuwezesha mwanamke kujikwamua kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Hata hivyo mkuu wa wilaya ametoa wito kwa wadau wote kuwekeza katika masuala ya wanawake ili kuhamasiaha na kuharakisha maendeleo ya taifa na jamii kwa ujumla kama ilivyo katika kauli mbiu ya maadhimishio ya siku ya wanawake duniani kwa mwaka 2024/2025.
Mwenyekiti wa mtandao wa polisi wanawake mkoa wa Kigoma akizungumza na waadishi wa habari katika kikao cha ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kilichofanyika katika ukumbi wa RAS
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa mtandao wa polisi wanawake (TPF) ASP Rosemary Kitwala amesema ni muhimu wanawake kutoa taarifa za uhalifu zinazofanywa na waume zao kwa usiri ili kuhakikisha haki inatendeka na kuwaasa wanaume kufika katika dawati la jinsia na Watoto ili kutoa kero zao endapo wananyanyasika.
Kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kimkoa yatafanyika katika kata ya Makere halamsahuri ya wilaya ya Kasulu mnano tarehe 08 Machi 2024 na kwa halmashuri ya wilaya ya Kigoma yatafanyika kata ya ziwani Kijiji cha Mtanga mnamo tarehe 06 Machi 2024.