MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA AMEKAGUA MADARASA YA UVIKO 19.
Posted on: November 21st, 2021Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bi. Rose Manumba amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa madarasa chini mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19. Mkurugenzi ametembela shule zote zinazojenga vyumba vya madarasa na jumla ya vyumba 69 vya madarasa vinajengwa kwa gharama ya Tsh. Bilioni 1.38 katika Halmashauri hiyo. Ujenzi umefikia hatua mbalimbali ikiwa ni hatua ya kupaua na baadhi ukamilishaji wa Boma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bi. Rose Manumba (wa tatu kutoka kushoto) akiwa pamoja na wataalamu kutoka Halmashauri hiyo katika ukaguzi wa ujenzi vya vyumba sita (6) vya madarasa katika shule ya sekondari Mgawa iliyopa Kata ya Mahembe siku ya tarehe 20 Novemba, 2021.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bi. Rose Manumba (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na wataalamu kutoka Halmashauri hiyo katika ukaguzi wa mradi ujenzi wa vyumba saba (7) vya madarasa katika shule ya sekondari Kasima iliyopo Kata ya Simbo siku ya tarehe 20 Novemba, 2021.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bi. Rose Manumba (wa nne kutoka kulia) akiwa pamoja na wataalamu na walimu wa shule ya sekondari Mwandiga wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa vyumba vitatu (3) vya madarasa katika shule hiyo iliyopo kata ya Mwandiga siku ya tarehe 20 Novemba, 2021.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bi. Rose Manumba (wa pili kutoka kulia) na wataalamu kutoka Halmashauri hiyo wakishiriki kusogeza mchana pamoja na vibarua wa ujenzi katika shule ya sekondari Kaseke iliyopo Kata ya Simbo siku ya tarehe 20 Novemba, 2021.
Sehemu ya jengo la vyumba sita (6) vya madarasa katika shule ya sekondari Mgawa iliyopo Kata ya Mahembe likiwa hatua ya kufunga Rinta na kukamikisha Boma hadi kufikia tarehe 20 Novemba, 2021. Gharama ya vyumba hivyo ni Tsh. Milioni 120.