MICHE YA KAHAWA ZAIDI YA MILLIONI 4 YAZALISHWA KIGOMA DC
Posted on: May 9th, 2024Halmashauri ya wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma imefanikiwa kuzalisha miche milioni nne ya kahawa aina ya compact kupitia taasisi ya utafiti wa zao la kahawa nchini ( TACRI) ili kuongeza uzalishaji.
Afisa kilimo wa kata ya Kalinzi Richard Mwakyusa amesema mbegu hizo zitaongeza uzalishaji kutoka kilo 400 za kahawa ya zamani aina ya arabica kwa hekali moja mpaka kilo 1800 kwa aina hii mpya ya mbegu.
Amesema uzalishaji huo utaleta mapinduzi kwa wakulima wa zao hilo kwa kuongeza kwa kufanya kilimo hicho kuwa chenye tija kwa kuongeza kipato na kuboresha maisha yao.
Afisa kilimo amefafanua kuwa kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2023/2024 jumla ya wakulima 5000 wamelima kwa kutumia mbegu hizo, miongoni mwao wakiwa wakulima 3600 kutoka wilaya ya Kigoma na wengine kutoka katika wilaya jirani ya Buhigwe.
Halmashauri ya wilaya ya Kigoma ninkongwe katika kilimo cha kawaha kwa zaidi ya miaka 100
Akizungumza mkulima Samola Soda amesema aina hiyo ya miche ni nzuri kwa mkulima kwani haiozi na si rahisi kupata magonjwa na kwamba huanza kuzaa kuanzia ikiwa na mwaka mmoja na nusu.