HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA YAFANYA MAFUNZO ELEKEZI YA UTOAJI WA KINGATIBA KWA JAMII
Posted on: November 22nd, 2023Na Mwandishi Wetu: Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma imefanya mafunzo elekezi kwa watoa huduma za afya na walimu juu ya umezeshaji kingatiba kwa watoto wenye umri miaka 5 hadi 14 ili kujikinga na magonjwa ya minyoo ya tumbo na kichocho. Katika Mkoa wa Kigoma, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI inaendesha zoezi la umezeshaji vidonge vya kingatiba kwa ajili ya kudhibiti magonjwa ya minyoo ya tumbo na Kichocho katika Halmashauri nane za mkoa wa huo huku Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ikiwa ni miongoni wa Halmashauri zinazoendesha zoezi hilo. Akiongea katika mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mhe. Salum Kalli, amesema magonjwa hayo zamani yalikuwa hayapewi kipaumbele, lakini sasa Serikali inayapa kipaumbele na ndiyo maana imetoa dawa ambazo ni kingatiba.
Pichani juu: Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mhe. Salum Kalli akiongea na washiriki wa mafunzo hayo.
Pichani juu: Washiriki wakiwa katika mafunzo elekezi
Akiongea katika mafunzo hayo mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dr. Jackson Elieza kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma amesema Wizara Afya kupitia mpango wa taifa wa kudhibiti magonjwa yasiyopewa kipaumbele, imedhamiria kutekeleza mpango huo ili kuhakikisha watanzania wanakuwa na afya bora kwa kuwakinga dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika. Amesisitiza kuwa ili malengo ya serikali yaweze kufikiwa, wataalamu wa Afya, walimu pamoja na jamii kwa ujumla inapaswa kushirikiana katika kuwatambua walengwa na kuhakikisha wanafikiwa kisha kupatiwa huduma.
Zoezi la ugawaji kinga tiba ya magonjwa ya minyoo ya tumbo na Kichocho limeanza kutekelezwa kuanzia Novemba 23 hadi 25 Desemba 2023 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma. Mafunzo hayo pia yamehudhliwa na waratibu wa elimu katika Kata.
Pichani juu: Washiriki wakiwa katika mafunzo elekezi
Pichani juu: Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma akiongea na washiriki wa mafunzo
Pichani juu: Mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dr. Jackson Elieza akitoa maelezo kuhusu utoaji wa Kingatiba kwa washiriki.
Pichani juu: Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigoma Ndg. Mganwa Nzota akisema jambo wakati wa mafunzo