MAAFISA UGANI WATAKIWA KUFANYA KAZI YENYE TIJA KWA JAMII
Posted on: March 3rd, 2024- Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kigoma, Ndugu Chiliku Hamisi Chilumba amewataka maafisa ugani kufanya kazi yenye tija kwa jamii.
Akifungua kikao kazi cha Divisheni ya kilimo, ufugaji na uvuvi kilicho wahusisha maafisa ugani wa vijiji,kata na wilaya , kilichofanyika jana tarehe 1,machi, 2024, katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kigoma, Amewataka maafisa hao kuacha utoro wa reja reja badala yake wajikite kuwahudumia wananchi katika maeneo yao ili uwepo wao uwe na tija kwa jamii zinazo wazunguka.
Aidha mkuu wa divisheni ya kilimo ndugu Fedrick Mtui amewataka maafisa hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali watumie nafasi walizonazo kufanya kazi kwa kuwasadia wananchi kwani wao ni nguzo muhimu katika Uchumi wa taifa
Maafisa ugani wakisikiliza kwa makini maelekezo kutoka kwa viongozi wao
Wakuu wa section wakisikiliza uwasilishwaji wa taarifa za mwezi kutoka kwa maafisa ugani kata na vijiji.