MAAFISA UANDIKISHAJI KATA JIMBO LA KIGOMA KASIKAZINI WANOLEWA
Posted on: July 13th, 2024Tume huru ya taifa ya Uchaguzi imetoa mafunzo kwa maafisa uandikishaji wa halmashauri ya wilaya ya Kigoma jimbo la Kigoma Kaskazini ili kuwajengea uwezo wa kuwafundisha waandikishaji ngazi ya kituo.
Akizungumza wakati wa mafunzo afisa uandikishaji wa halmashauri ya wilaya ya Kigoma Linus Skainda amesema mafunzo hayo yatafanyika kwa muda wa siku mbili, tarehe 13/14 Julai 2024 katika ukumbi wa Nzimano uliopo mjini Kigoma na kisha mafunzo ngazi ya kituo yataanza kufanyika tare 16/17 Julai 2024.
Maafisa Uandikishaji wa kata wakiapishwa wakati wakipatiwa Mafunzo ya uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura
Skainda ameeleza kuwa majukumu mbalimbali yameshafanyika katika uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura ikiwemo kutembelea vituo vyote vya uchaguzi 132, kufanya mikutano na vyama vya siasa 19 vilivyopo katika Jimbo hilo na kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa kujitokeza kwaajili ya kuboresha taarifa zao.
“Maafisa uandikishaji wameaapishwa Leo tarehe 13 Julai, 2024 chini ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Kigoma Eva Mushi, maafisa hawa baada ya mafunzo watawafundisha maafisa ngazi ya vituo, lakini pia Leo tumeanza matangazo kwa njia ya magari na yatakamilika mwisho wa zoezi tarehe 27 Julai 2024” amefafanua Skainda.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, mratibu wa uboreshaji wa Daftari mkoa, Hussein Moshi amewataka washiriki kuelewa vizuri kila wanalofundishwa kwa sababu zoezi hilo ni maalumu na linahitaji umakini katika utekelezaji wake
Amewaasa kuwa wakati wa uboreshaji wa taarifa hizo watumie lugha nzuri na kuwaelekeza wananchi vizuri ili wasiharibu kazi na sifa ya zoezi hilo na kwamba kokote watakapokutana na changamoto katika vituo watoe taarifa kwaajili ya utatuzi wa changamoto hizo