MAADHIMISHO YA SIKU 365 ZA MH. SAMIA SULUHU HASSAN MADARAKANI

Wilaya ya Kigoma imeadhimisha mwaka mmoja wa uongozi wa Mh. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Maadhimisho hayo yameandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wakishirikiana na wadau mbalimbali wa Wilaya ya Kigoma. Maadhimisho hayo yamefanyika katika uwanja wa Mwanga Community Centre katika manispaa ya Kigoma Ujiji huku mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mh. Thobias Andengenye. Maadhimisho hayo yameudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa, taasisi za Serikali na zisizo za Serikali, viongozi wa dini, watumishi wa Serikali pamoja na wananchi wa Wilaya ya Kigoma.
Pichani juu: Viongozi wa Wilaya ya Kigoma wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mh. Thobias Andengenye (Katikati mwenye Suti)
Wananchi wakiwa wamejitokeza kuadhimisha siku 365 za Mh. Samia Suluhu Hassan madarakani.
Dhumuni la maadhimisho hayo ni kuonesha shughuli za maendeleo zilizofanyika katika Wilaya ya Kigoma kwa kipindi cha mwaka mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania madarakani. Sambamba na maadhimisho hayo, pia kulikuwepo na maonesho kutoka Taasisi zinazopatikana Wilaya ya Kigoma pamoja na vikundi mbalimbali vya ujasiliamali kutoka Halmashauri mbili zinazopatika katika Wilaya ya Kigoma.
Pichani juu: Banda la TANAPA katika maadhimisho ya siku 365 za Mh. Samia Suluhu Hassan madarakani
Mkuu wa Mkoa Mh. Thobias Andengenye (Katikati mwenye Tai Nyekundu) akipatiwa maelezo kuhusu ufugaji wa Samaki kutoka kwa Mtaalamu wa Uvuvi Bw. Jumanne Yassini (Wa tatu kutoka kulia mwenye Shati Nyeupe). Kushoto kwa Mkuu wa Mkoa ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Ester Alexander Mahawe akifuatiwa na Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Kilumbe Shaban Ng'enda
Maadhimisho hayo ya mwaka mmoja wa uongozi wa Mh. Samia Suluhu Hassan yaliambatana na burudani mbalimbali kutoka vikundi tofauti tofauti vinavyopatikana Wilaya ya Kigoma pamoja na mwanamuziki Peter Msechu kutoka Dar es Salaam.
Pichani juu: Wananchi wakicheza na mwanamuziki Peter Msechu
Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza wakatai wa Maadhimisho ya Siku 365 za Mh. Samia Suluhu Hassan madarakani
Katika taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Ester Alexander Mahawe, kwa siku 365 jumla ya miradi yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 181 imeelezwa kutekelezwa na mingine ikiendelea kutekelezwa katika Wilaya ya Kigoma. Miradi hiyo ni katika sekta ya Elimu, Afya, Kilimo, Barabara, Mikopo kwa Vijana na wanawake, Maji, masuala ya kiutawala pamoja na sekta zingine katika Wilaya ya Kigoma.
Picha juu: Mkuu wa Mkoa Mh. Thobias Andengenye akiongea na wananchi wa Wilaya ya Kigoma katika viwanja vya Mwanga Community Cetre wakati wa maadhimisho ya siku 365 za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pichani juu: Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Mh. Joseph Nyambwe akiongea na wananchi wa Wilaya ya Kigoma katika viwanja vya Mwanga Community Cetre wakati wa maadhimisho ya siku 365 za Rais wa Jamhuri ya Muungano
Pichani juu: Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bi. Rose Robert Manumba akiongea na wananchi wa Wilaya ya Kigoma katika viwanja vya Mwanga Community Cetre wakati wa maadhimisho ya siku 365 za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika maadhimisho hayo, Wilaya ya Kigoma ilitoa zawadi kwa Mh. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufikia mafanikio mbalimabli kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu aingie madarakani.
Mkuu wa Mkoa Mh. Thobias Andengenye (Katikati) pamoja na viongozi wengine wakiwa wameshikilia zawadi ya picha kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.