• Webmail
  • Maswali ya Mara kwa mara
  • Wasiliana nasi
Kigoma District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali watu
    • Planning and Management
    • Finance and Accounts
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Procurement and Supply
    • Economy and Production
    • Miundombinu
    • Local Government
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Guidelines
    • Procedures
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Media Center
    • Habari
    • Matangazo kwa umma
    • Maktaba
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Videos

KIKAO CHA KAMATI WA LISHE KWA ROBO YA NNE APRILI-JUNI, 2023 CHAFANYIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA

Posted on: July 13th, 2023

Kamati ya Lishe ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma imefanya kikao Jumuishi cha Lishe na kujenga uwezo kwa wajumbe wa Kamati ya Lishe ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma. Kikao hicho pia kimetumika kuwasilisha utekelezaji wa shughuli za Lishe kwa kipindi cha robo ya nne  ya April - Juni, 2023. Kikao hicho kimefanyika tarehe 13 Julai, 2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.  


Pichani juu: Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Salum Kalli (Katikati) akimsikiliza

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bi. Rose Manumba (Aliyesimama).

Kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Dr. Maria Gekondo


Kikao kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Salum Kalli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Lishe ya Wilaya. Katika ufunguzi wake Mh. Mkuu wa Wilaya amesisitisha elimu na ufuatiliaji wa afua za lishe ili kuwa na jamii yenye afya bora. Kikao hicho pia kimehudhuliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bi. Rose Robert Manumba. Katika kutekeleza afua za Lishe, Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bw. James Swai amebainisha kutolewa kwa bajeti ya Lishe inayotokana na mapato ya ndani katika afua za Lishe.


Pichani juu: Wajumbe wa Kamati ya Lishe wakiwa kwenye kikao.


Miongoni mwa mambo ambayo Mratibu wa Lishe ameweza kuyafanya katika kipindi cha robo ya tatu Januari - machi, 2023 ni pamoja na: Utoaji wa dawa za kuongeza wekundu wa damu (FeFo) kwa wanawake wajawazito waliohudhuria clinic, Kupima uwepo wa madini joto kwenye chumvi inyouzwa sokoni na inayotoka kwenye jamii kupitia wanafunzi shuleni, kufanya Siku ya Afya na Lishe (SALiKi) katika vijiji 45, Kushiriki kufanya kampeni ya kitaifa ya mwezi wa afya na lishe ya mtoto n.k. 


Pichani juu: Mratibu wa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bw. James Swai


Kikao hicho pia kilihudhuriwa na wataalamu wa idara ya afya kutoka ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma pamoja na Mratibu wa Lishe kutoka OR-TAMISEMI Bw. Mwita Waibe amabaye pia alitoa maelekezo ili kuweza kufanikisha Afua za Lishe. Bw. Mwita Waibe alisisitiza umuhimu wa kuwa na data zenye ubora ili ziweze kusaidia katika maamuzi sahihi.

Pichani juu: Mratibu wa Lishe kutoka OR-TAMISEMI akiongea na kamati ya Lishe ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.

Latest Announcements

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MUDA

    read more
  • WRITTEN INTERVIEW RESULTS MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA PILI

    read more
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA VIJANA, WANAWAKE NA WATU WENYE ULEMAVU

    read more
  • View More

Habari M-pya

  • WALENGWA WA KAYA MASKINI WAHIMIZWA KUENDELEZA UJUZI NA MIRADI WALIYOANZISHA
  • JESHI LA MAGEREZA KWITANGA LAFANYA USAFI HOSPITALI YA WILAYA YA KIGOMA LIKIFANYA MAADHIMISHO YA WIKI YAKE
  • SERIKALI YAKABIDHI MABOTI MAWILI YENYE THAMANI YA TSH MILIONI 100 KWA AJILI YA KUIMARISHA DORIA ZIWA TANGANYIKA
  • NG’OMBE 7,000 KUCHANJWA DHIDI YA HOMA YA MAPAFU KIGOMA DC
  • CHMT KIGOMA DC YAFUATILIA KWA UKARIBU HUDUMA ZA AFYA MWAMBAO WA ZIWA TANGANYIKA
  • More

Wasiliana nasi

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
THE DISTRICT EXECUTIVE DIRECTOR
Postal Address: P.O.Box 332, KIGOMA
Telephone: 028 2804865
Barua pepe: ded@kigomadc.go.tz
Mobile: 028 2804865
P.O.Box 332 KIGOMA
Postal Address: MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA KIGOMA
Telephone: 028 280 271 9
Barua pepe: ded@kigomadc.go.tz
Mobile: +255752337486

Tovuti zinazo fanana

  • Kigoma Ujiji Mc
  • Halmashauri ya Wilaya Uvinza
  • Halmashauri ya Wilaya Buhigwe
  • Halmashauri ya Wilaya Kasulu
  • Halmashauri ya Mji wa Kasulu
  • Halmashauri ya wilaya Kibondo
  • Halmashauri ya wilaya Kakonko

Tovuti Zinazo husiana

  • OFISI YA RAIS TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI (NECTA)
  • WIZARA YA UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  • MKOA WA KIGOMA
  • TOVUTI YA TAIFA
  • MFUMO WA MADENI YA WATUMISHI SERIKALINI
  • SALARY SLIP PORTAL

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2024GWF . All rights reserved.

  • Vigezo
  • Sera za Usiri
  • Maswali ya Mara kwa mara
  • Ramani