KATIBU TAWALA WA WILAYA YA KIGOMA AAGIZA KODI YA DAGAA IBAKI MOJA
Posted on: March 8th, 2024
Na mwandishi wetu
Katibu wa tawala wa halmshauri ya wilaya ya Kigoma Mgwanwa Nzota, ameziagiza mamlaka zinazohusika na tozo za mazao ya samaki na dagaa kukubaliana aina moja ya tozo kwa wajasiamali wa bidhaa hizo ili kuondoa usumbufu.
Agizo hilo amelitoa leo tarehe 6 Machi 2024 katika maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani ambayo kiwilaya yamefanyika kata ya Ziwani, kijiji cha Mtanga, baada ya wanawake wa kata hiyo kulalamika namna wanavyoumizwa na ukusanyaji wa tozo kutoka malmlaka tofauti tofauti.
“Hatuna sababu ya kuwasumbua akina mama wajasiriali kwa namna tunavyowasumbua, kama kuna haja ya wao kulipia ushuru halmashauri au tumeona kuna haja ya wao kulipia BMU sisi ndio serikali , tukae pamoja, tukokotoe pamoja huo ushuru na huyu mwanamke awe analipa ushuru mmoja tu, sio alipie kwenye kila malamka” Amesema Katibu tawala
Awali wanawake hao walilalamika kutozwa tozo na mgambo, wasimamizi wa rasilimali za ziwa (BMU),na malaka za halmshauri jambo ambalo linafanya waone kuwa ni usumbu na linawafanya waone kudhulumiwa haki ya kufanya kazi kwa uhuru.
Akizungumza kwa niaba ya wanawake hao, Zuwena Rashid, amesema endapo agizo hilo litatekelezwa kwa wakati litatatua hali ya unyanyasaji inayoendelea katika biashara hiyo.