HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA YAFANYA KIKAO CHA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE

Na Mwandishi wetu:
Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma imefanya kikao cha Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe chini ya Mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Salum Kalli. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kikiwahusisha Maafisa Watendaji wa Kata, wakuu wa Idara na Vitengo pamoja, Mkuu wa Wilaya pamoja na viongozi wengine wa Wilaya.
Pichani juu: Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Salum Kalli akishikiri kikao
cha Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Salum Kalli amewasisitiza Maafisa Watendaji wa Kata kuendelea kuwaibua watoto wenye changamoto ya lishe. Mkuu wa Wilaya amesisitiza Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kuendela kutenga bajeti Shilingi elfu 1 kwa kila mtoto kwa ajili ya lishe. Pia ameendela kuwakumbusha wataalamu na viongozi kuendelea kutoa elimu ya lishe bora kwa jamii ili kupata jamii yenye lishe bora.
Kikao hicho kimepitia mkataba wa lishe ili kuona wapi Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma imefanikiwa na wapi bado kuna changamoto na kuziwekea mikakati ya kuzitatua ili kufikia malengo.
PichanI juu: Wajumbe wakishiriki kikao cha utekelezaji wa mkataba wa lishe
katika halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Wakihojiwa kwa nyakati tofauti baadhi ya maafisa watendaji wa Kata wamekili kuwepo changamoto mbalimbali ambazo zinakwamisha kufikia malengo sahihi, lakini wanaendela kutoa elimu kwa jamii ili ione umuhimu wa lishe bora na pia jamii ishiriki moja kwa moja ili kufikia malengo.
Pichani juu: Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
akiongea na washiriki wa kikao cha utekelezaji wa Mkataba wa lishe.
Nae Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bw. James Swai ameushukuru uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwa kuendela kutenga bajeti na kutoa shilingi 1 kwa kila mtoto ili kutekeleza mkataba wa lishe. Lengo ni kuhakikisha jamii inapata lishe bora na kupunguza na kuwaondoka kabisa tatizo la utapiamlo.
Pichani juu: Wajumbe wa kikao wakiendelea na kikao katika
ukumbi wa Halmashauri ya Wialya ya Kigoma
Pichani juu: Wajumbe wa kikao wakiendelea na kikao katika
ukumbi wa Halmashauri ya Wialya ya Kigoma