HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA YAFANYA KIKAO CHA TATHMINI YA MKATABA WA LISHE KATIKA ROBO YA JULAI-SEPTEMBA, 2023
Posted on: November 14th, 2023Na Mwandishi Wetu:
Tarehe 12 Novemba, 2023 Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma imefanya kikao cha tathmini ya mkataba wa Lishe. Kikao hicho kinachowahusisha Watendaji wa Kata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, pamoja na baadhi ya wataalamu wa Halmashauri, kimefanyika chini ya Mwenyekiti wa kamati ya Lishe ya Wilaya aliyewakilishwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigoma Bw. Mganwa Nzota.
Katika ufunguzi wa kikao hicho Bw. Mganwa Nzota ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigoma amewakumbusha Watendaji wa Kata kutekeleza mkataba huo kwa ufanisi ili kufikia malengo. Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigoma amesisitiza ushirikiano wa watendaji wa Kata, wataalamu wa afya, wahudumu wa ngazi ya jamii pamoja na wadau wengine ili kuhakikisha mkataba wa Lishe unatekelezeka kwa ufanisi. Kwa upande wao Watendaji wa Kata wameomba mafunzo mbalimbali ya wahudumu wa ngazi ya jamii yatolewe kwa mzunguko ili kila muhudumu wa ngazi ya jamii apate utaalamu na kuondoa hali ya wahudumu wachache kujirudia kupata mafunzo kila yanapotolewa.
Pichani juu: Watendaji wa Kata na baadhi ya wataalamu wa Halimashauri wakiwa kwenye kikao cha tathmini ya mkataba wa Lishe.
Watendaji wa Kata wamehaidi kushawishi wazazi na jamii kwa ujumla ili wanafunzi waweze kupata chakula shuleni ikiwa ni sehemu ya mkataba wa Lishe. Katika kikao hicho pia mikakati imewekwa ili kuhakikisha mkataba wa Lishe unatekelezwa kwa ufanisi. Miongoni mwa mambo yaliyopangwa ni kuendelea kushawishi wazazi ili kuchangia chakula mashuleni. Pia shule zenye uwezo wa kuanzisha mashamba madogo madogo watumie fulsa hiyo ili kuzalisha chakula kwa ajili ya chakula mashuleni.
Pichani juu: Mtendaji wa Kata ya Bitale Bi. Betrida Rusigwa (Aliyesiama) akichangia mada kwenye kikao cha tathmini ya mkataba wa Lishe.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigoma Bw. Mganwa Nzota ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kigoma amewaomba wazazi na wananchi kwa ujumla wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kutoa ushirikiano kwa walimu na viongozi mbalimbali ili wanafunzi waweze kupata chakula shuleni ikiwa ni sehemu ya kutekeleza mkataba wa Lishe. Pia shule zenye uwezo wa kulima mashamba, wawezeshwe ili waweze kuzalisha chakula kwa ajili ya wanafunzi wanapokuwa shuleni.
Pichani juu: Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigoma Bw. Mganwa Nzota akisoma hotuba katika kikao cha tathmini ya mkataba wa Lishe.
Kikao kimeweka mikakati na namna ya kutekeleza mikakati hiyo kwa wakati ili kufikia mafanikio na kulingana viasharia vya mkataba wa Lishe. Kupitia hotuba yake Mkuu wa Wilaya ya Kigoma iliyosomwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigoma, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma ameagiza watendaji wa Kata kusimamia mkataba wa Lishe. Pia Mkuu wa Wilaya ya Kigoma kupitia hotuba yake amewataka Watendaji wa Kata kufanya ufuatiliaji na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe.
Pichani juu: Wajumbe wakifuatilia taarifa ya lishe kwenye kikao cha tathmini ya mkataba wa Lishe cha Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
Pichani juu: Mtendaji wa Kata ya Mwandiga Bw. Kashoba Ally Kashoba (aliyesimama) akichangia mada kwenye kikao cha tathmini ya mkataba wa Lishe cha Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
Pichani juu: Wajumbe wakichangia mada kwenye kikao cha tathmini ya mkataba wa Lishe cha Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma