HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA IMETOA MOTISHA KWA WALIMU WA SHULE ZILIZOFANYA VIZURI KATIKA MITIHANI YA DARASA LA SABA NA DARASA LA NNE MWAKA 2023
Posted on: March 6th, 2024Na mwandishi wetu
Halmashauri ya wilaya ya Kigoma imetoa takribani milioni 12,000,000 kama motisha kwa walimu, shule na kata zilizofanya vizuri katika mtihani ya kuhitimu darasa la saba na mtihani wa kujipima wa darasa la nne kwa mwaka 2023.
Akitoa motisha hiyo kaimu mkurugenzi ambaye pia ni afisa elimu msingi wa halmsahuri hiyo Kassim Mtili amesema motisha hizo zimetolewa kwa lengo la kuhimiza ufaulu, na kuleta ushindani katika sekta ya elimu itakayoinua hamlashauri hiyo kutoka nafasi ya tatu waliyoshika mwaka 2023 na kushika nafasi ya kwanza kwa mwaka 2024.
“Tunafurahi kuona halmshauri yetu imeshika nafasi ya tatu kati ya ya halmashauri nane zilizopo mkoani humu, nawaomba sana tufanye kazi kwa bidii ili tuweze kushika nafasi ya kwanza kimkoa kwakuwa uwezo tunao na nia ya kufanya vizuri tunayo” Amesema Mtili.
Walimu wakiwa kwenye kikao Cha kupokea motisha ukumbi wa SHULE ya sekondari mwandiga
Amefafanunua kuwa mwaka 2023 halmashauri hiyo imefanya kuongeza ufaulu kwa asilimia 6.79 kutoa asilimia 80 mwaka 2022 hadi kufikia asilimia 86.79 mwaka 2023.
Akitoa ufafanuziwa motisha hizo, afisa elimu taaluma, Edo Madyane, amesema zimegawiwa katika makundi matatu ambapo kundi la kwanza ni kwa shile zenye watahiniwa kuanzia mmoja mpaka 40, kundi la pili lenye watahiniwa kuanzia 41-99, na kundi la tatu lenye watahiniwa 100-160
Afisa Elimu vifaa na takwimu kushoto Katikati Katibu wa chama Cha walimu Wilaya ya Kigoma na kulia ni Afisa Elimu ya watu wazima wakishiriki Katika zoezi la kutoa motisha kwa walimu
Amesema shule zilizoibuka washindi kwa kushika nafasi ya kwanza kutoka katika makundi hayo ni shule ya msingi Kisozi,kundi la kwanza, shule ya msingi Kiganza na Mkigo kundi la pili na shule ya msingi Mgogo iliyopo kata ya Kalinzi katika kundi la tatu.
Kwa upande wake Katibu wa tawala wa halmshauri ya wilaya ya Kigoma Mgwanwa Nzota, ametoa ahadi kuwa endapo halmashauri ya wilaya ya Kigoma itweza kushika nafasi ya kwanza kiwilaya ofisi yake itatoa zawadi ya shilingi miloni tano na kwa shule zitakofanya vizuri atatoa zawadi ya milioni moja.
Akiongea mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kiganza ambaye shule yake imepokea tuzo 6, Gerlad Kizeba amesema wataendelea kufanyia kazi mikakati iliyotolewa na halmashauri hiyo ili kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi kwa kushirikiana na wazazi, walimu, wanafunzi na wadau wengine wa elimu
Mikakati iliyowekwa na halmashauri hiyo ili kufikia malengo ya kushika namba moja ki mkoa ni kufanya usajili yakinifu kwa kuzingatia mahudhurio, kukamilisha mada za ufundishaji kwa darasa la saba na la nne ifikapo mwezi Juni, kufanya mtihani wa majaribio kila mwezi, kuweka kambi ya masomo na kufanya mtihani wa ujirani mwema.