Mifugo na Uvuvi
Sekta ya mifugo na Uvuvi imekuwa na mchango mkubwa katika shughuli za kiuchumi na kutegemewa na wananchi katika kujiongezea kipato na kitoweo. Mifugo inayofugwa wilayani ni Ng’ombe, Mbuzi, Kondoo, Nguruwe, kuku, Bata na Kanga. Mpaka kufikia June 2016 idadi ya mifugo iliyokuwa ni Ng’ombe 7,697, Mbuzi 30,230, Kondoo 10,697, Nguruwe 2,623, Mbwa 3,460, Kuku 144,062 na Bata 4,500.
Hali ya uvuvi katika eneo la Halmashauri ya wilaya ya Kigoma imekuwa ikipungua kila mwaka, hali hiyo imechangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi, uvunaji wa samaki uliopitiliza kutokana na kuongezeka kwa mahitaji na idadi ya watu wanaotegemea rasilimali za uvuvi. Hali hii imepelekea baadhi ya aina ya samaki kutopatikana tena, Uvuvi haramu nao umechangia katika kupungua kwa mazao yatokanayo na uvuvi. Ili kunusuru uvuvi haramu halmashsuri ya wilaya huwa inafanya doria katika ziwa na nchi kavu juu ya uvuvi haramu na kukamata na kulipisha faini kwa mazao yote yanayokuwa yamevuliwa kinyume cha sheria.