Halmashauri ya wilaya inaendelea na mkakati wa uwezeshaji wa wananchi kiuchumi ikiwemo kusajiri vikundi vya ujasiriamali, kutoa elimu ya ujasiriamali (elimu ya biashara), kutoa mikopo kwa vikundi vya vijana na wanawake, kufuatilila urejeshaji wa mikopo na kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa vikundi vya ujasiriamali.
Halmashauri imeendelea na uhamasishaji wa uundaji wa SACCOs na utumiaji wa huduma za fedha zinazotolewa na SACCOs. SACCOs zilizotembelewa ni SACCOS za Rusunu na Tuungane katika kata ya Nkungwe; SACCOS ya kijiji cha kigalye -Kata ya Ziwani; JUHUDI SACCOS katika kijiji cha Mtanga -Kata ya Ziwani; TULIHAMWE SACCOS katika kijiji cha nyarubanda -Kata ya Nyarubanda; na TANGANYIKA SACCOS katika Kata ya Kagunga.
Halmashauri inaendelea kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa vikundi vya ujasiriamali vya wanawake na vijana ili kutoa ushauri na elimu elekezi juu ya ujasiriamali, uwekaji wa akiba, mikopo na sifa za kikundi hai. Jumla ya vikundi 191 katika kata zote 16 za Halmashauri ya Wilaya zilitembelewa na takribani watu 4,269 (Wanaume 1845 na Wanawake 2424) walipata elimu iliyokusudiwa. Kwa mwaka 2015/16 Halmashauri imetoa mikopo kwa vikundi 7 vya vijana yenye thamani ya shilingi TZS 19,000,000/= Katika fedha hizo, shilingi milioni kumi na nne zilipokelewa toka Serikali Kuu na shilingi milioni 5 ni mchango wa Halmashauri. Vikundi vilivyopokea mikopo ni kama ifuatavyo;
Vikundi Vijana Vilivyopokea Mkopo 2015/16
JINA LA KIKUNDI |
KIJIJI |
KIASI KILICHOTOLEWA |
SACCOS ya Vijana
|
Kidahwe
|
8,000,000/= |
Sanaa Two Times –Youths
|
Mwandiga
|
6,000,000/= |
VIWASE Vijana
|
Mkabogo
|
1,000,000/= |
Kikundi cha Walemavu (KIWAWAKI)
|
Kalinzi
|
1,000,000/= |
Tanganyika Beekeeping
|
Kagongo
|
1,000,000/= |
Tuamke Women Group
|
Msimba
|
1,000,000/= |
KIYODEO (Vijana)
|
Mwandiga
|
1,000,000/= |
JUMLA |
|
19,000,000/= |
Halmashauri imeendelea kutekeleza mradi wa Tasaf awamu ya III ambao ulizinduliwa mnamo mwezi wa Aprili 2014 ukiwa na lengo kuu la kunusuru kaya masikini, toka mradi uzinduliwe Halmashauri imefanikiwa kutekeleza shughuli zifuatazo. Yametolewa mafunzo kwa viongozi na watendaji katika ngazi mbalimbali, umefanyika utambuzi wa walengwa kwenye ngazi za vijiji, uandikishaji wa walengwa, uhawilishaji wa fedha kwa walengwa ambapo kaya masikini 5183 zinanufaika na ruzuku zinazotolewa kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini.