FULSA ZA UWEKEZAJI IDARA YA MIFUGO
UFUGAJI WA KUKU
Halmashauri ya Kigoma ina fulsa katika ufugaji wa kuku, kwa sasa hivi, idadi ya kuku ni zaidi ya 144,069. Fulsa na zilizopo katika ufugaji kuku ni pamoja na kuwepo kwa vyakula vingi vya kuku kama Mahindi, dagaa, mashudu ya mise, pumba, chumvi, mbaazi, magamba ya konokono na bidhaa nyingine za viwandani, zinazopatikana madukani.
Fulsa nyingine iliyopo katika ufugaji kuku ni pamoja na kuwepo kwa soko la kutosha la kuku ndani na nje ya mkoa kwa bei nzuri.
Changamoto wanayokabiliana wafugaji ni ukosefu wa vifaranga bora wa kuku, kiasi ambacho wafugaji wengi wanafuata vifaranga Mwanza au Dar-es-Salaam.
UFUGAJI WA NGURUWE
Halmashauri ina zaidi ya nguruwe 2,603 lakini bado kuna fulsa nzuri ya uwekezaji katika ufugaji wa nguruwe, kwa sababu ya upatikanaji wa chakula kama mashudu ya mise, mahindi, mihogo, viazi, ndizi, pumba nk
Changamoto iliyopo ni ukosefu wa mbegu bora ya nguruwe pamoja na soko la nguruwe na mazao yake.
UFUGAJI WA NG`OMBE WA MAZIWA
Halmashauri ina jumla ya ng`ombe 360 wa maziwa, lakini bado kuna fulsa ya uwekezaji katika ufugaji wan g`ombe hao katika kata ya Kalinzi, Mkigo,Nyarubanda, Simbo, Mahembe na Kidahwe. Kata hizo zina malisho ya kutosha na fulsa ya kupanda majani, kwa ajili ya malisho. Vilevile vyakula vya ziada vinapatikana ndani na nje ya Halmashauri.
Changamoto iliyopo ni ukosefu wa mbegu bora za ng`ombe wa maziwa na soko la Maziwa.
KIWANDA CHA KUSINDIKA MAZIWA.
Halmashauri ina fulsa kubwa ya kuwa na uwekezaji katika kusindika maziwa,katika kata za Mungonya kwani maziwa yaliyopo vijijini hayana soko na hasa baada ya wafugaji kuhamia katika Halmashauri hii katika kata za simbo, Kidahwe na Matendo. Na vilevile kuna maziwa yanayozalishwa kutoka kwenye ng`ombe wa kisasa kata za Mkigo, Nyarubanda na Kalinzi, mazawa hayo hayana soko. Jumla ya maziwa yanayozalishwa kwa siku moja na kukosa soko, ni zaidi ya lita 4,000 katika Halmashauri ya kigoma na lita zaidi ya 5,000 yanatoka nje ya Halmashauri ya Kigoma.
3
UVUVI
KUWEKEZA KATIKA KUZALISHA VIFARANGA WA SAMAKI
Halmashauri ina wafugaji wenye mabwawa zaidi ya 16 ya kufugia samaki, katika kata mbalimbali
Changamoto kubwa iliyopo ni kupata fifaranga bora wa samaki. Kwa hali hiyo, kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na eneo maalumu kwa ajili ya kuzalishia watoto wa samaki.
KUWEKEZA KATIKA KUZALISHA BARAFU KWA AJILI YA KUSAFIRISHIA SAMAKI.
Kuna kipindi ambacho wavuvi wanavua samaki wengi na baadae samaki hao, wanakosa soko. Iwapo tutakua na uwekezaji wa kutengeneza barafu na masanduku ya kusafirishia samaki, itasaidia sana wafanyabiashara na wavuvi kuongeza kipato. kwani samaki na dagaa wabichi, watasafirishwa maeneo ambayo hayana mazao hayo, nje na ndani ya Halmashauri au nje ya nchi.
THE DISTRICT EXECUTIVE DIRECTOR
Postal Address: P.O.Box 332, KIGOMA
Telephone: 028 2804865
Mobile: 028 2804865
Barua pepe: ded@kigomadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Kigoma . Haki zote zimehifadhiwa