ZIARA YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA YA KIGOMA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA

Kamati ya Ulinzi na Usalama (KUU) ya Wilaya ya Kigoma imefanya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi katika Halmshauri ya Wilaya ya Kigoma. Miradi iliyotembelewa ni pamoja na maandalizi ya eneo la ujenzi wa ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, ujenzi wa hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, ujenzi wa maabara katika zahanati ya Mahembe iliyopo Kijiji cha Mahembe Kati na ujenzi wa matundu Matano ya vyoo katika zahanati ya Kizenga iliyopo Kijiji cha Kizenga.
Pichani juu: Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Ester Mahawe (mwenye nguo nyekundu) ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigoma akiwa na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigoma wakikagua maandalizi ya eneo la ujenzi wa ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Pichani juu: Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Ester Mahawe (kulia) ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigoma akioneshwa mchoro wa jengo la ofisi za Halmashauri zitakazojengwa. Anayemuonesha ni Mhandisi wa kampuni itakayojenga jengo hilo.
Katika kuwasilisha taarifa ya ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bi. Rose Robert Manumba amesema ujenzi huo ni wa jengo la gorofa moja na utafanyika kwa awamu, kiasi cha shilingi Bilioni 3.5 kinatarajiwa kutumika mpaka ujenzi utakapokamilika. Ujenzi huo unafanyika katika kijiji cha Mahembe Kati, Kata ya Mahembe. Akiwa na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Wilaya ya Kigoma, Mwenyekiti wa Kamati ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Ester Mahawe, amesisitiza umakini na usimamizi mzuri wa mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati. Jengo hilo linajengwa na kampuni iliyo chini ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mh. Ester Mahawe (katikati) ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigoma akiongea na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigoma.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigoma pia imetembelea mradi wa ujenzi wa hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na kuangalia kazi ya ujenzi unavyoendelea, Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kigoma amesisitiza juhudi ziongezeke ili mradi ukamilike kwa haraka.
Pichani juu: Mwonekano wa hatua ya jengo la utawala katika hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
Pichani juu: Mwonekano wa hatua ya jengo la maabara katika hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
Miradi mingine ambayo imetembelewa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigoma ni ujenzi wa matundu matano ya vyoo katika zahanati ya Kizenga na maabara katika zahanati ya Mahembe. Kamati ya ulinzi imeshauri kuongeza kasi ya ujenzi ili miradi imalizike kwa wakati
Pichani juu: Ukaguzi wa maabara katika zahanati ya Mahembe
Pichani juu: Ukaguzi wa matundu matano ya vyoo katika zahanati ya Kizenga