ZIARA YA KAMATI YA SIASA YA WILAYA

Kamati ya siasa ya Wilaya ya Kigoma Vijijini imefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma. Miongoni mwa miradi ilioyotembelewa ni pamoja na Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Madarasa ya UVIKO katika shule ya sekondari Kidahwe, Daraja la Samwa lililopo Kata ya Kidahwe ambalo lipo chini ya TARURA, Barabara ya Nkungwe iliyopo chini ya TARURA na mradi wa Maji uliopo Kijiji cha Chankabwimba ambao upo chini ya RUWASA. Kiongozi wa msafara wa ziara hiyo ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Kigoma VIjijini Ndg. Rashid Semindu amesisitiza kuendelea kuisimamia miradi hii vizuri ili iweze kuwanufaisha wananchi.
Pichani juu ni matukio mbaliambali wakati wa ziara ya Kamati ya siasa ya Wilaya ya Kigoma vijijini pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bi. Rose Robert Manumba (mwenue Gauni la Kitenge) wakiongea na wananchi waliojitokeza katika eneo ilipojengwa hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Pichani juu ni matukio mbaliambali wakati wa ziara Kamati ya siasa ya Wilaya ya Kigoma vijijini pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bi. Rose Robert Manumba (mwenye Gauni la Kitenge) katika mradi wa hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Pichani juu ni Muonekano wa majengo ya wagonjwa wa nje (OPD) na jengo la maabara katika Hosipitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Pichani juu ni ukaguzi wa mradi wa Maji kijiji cha Chankabwimba
Pichani chini ni matukio mbaliambali wakati Kamati ya siasa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bi. Rose Robert Manumba wakikagua mradi wa madarasa manne katika shule ya sekondali Kidahwe yaliyojengwa kwa fedha za UVIKO katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.