WASIMAMIZI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUFUATA SHERIA
Posted on: October 1st, 2024Msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Chiriku Chilumba amewataka wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa ngazi ya kata na vijiji kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na muongozo wa uchaguzi.
Chilumba ameyasema hayo katika mafunzo ya wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata na vijiji yaliyofanyika katika ukumbi wa “The Wallet” ambapo wasimamizi 46 wametoka katika ngazi ya vijiji, wasimamizi 16 kutoka ngazi ya kata na wasimamizi 10 kutoka ngazi ya halmashauri.
Wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wakipewa Mafunzo
Amesema kutokana na unyeti wa zoezi hilo wasimamizi hao wataongozwa na muongozo wa elimu ya mpiga kura kwaajili ya chaguzi wa serikali za mitaaa wa mwaka 2024 pamoja na kanuni za uchaguzi wa viongozi wa mamlaka ya serikali za mitaa ngazi ya vijiji, vitongoji na mitaa katika mamlaka za wilaya.
“Tushiriki kikamilifu katika zoezi hili nyeti kwaajili ya maslahi ya taifa, hakikisha unafanya kazi kikakimilifu katika nafasi yako, hakikisha yote unayotarajiwa kufanya kwa nafasi yako unayafanya, kinyume na hapo utaadhibiwa kulingana na sheria na kanuni, japo sitarajii kuona mnakwenda kinyume kwakuwa ninawaamini”Amesema Chilumba.
Katika hatua nyingine Chilumba amewataka wasimamizi hao kufanya uhamasihaji kwenye maeneo yao ili wananchi wajitokeze kujiandikisha katika daftari la mpiga kura kwakuwa inawapa haki ya kushiriki katika kupiga kura na kugombea nafasi mbalimbali.
“Wananchi wenye sifa wanahimizwa kujitokeza kujiandisha, na wenye sifa ya kuwa wagombea wajitokeze kuwania nafasi hizo kwakuwa inakuza demokrasia na kuhakikisha upatikanaji wa viongozi bora kwa aajili ya maendeleo ya taifa letu”Amesema Chilumba.
Kwa upande wake Linus Skainda, Msimamizi Msaidizi kutoka halmashauri ya wilaya ya Kigoma amewashauri wasimamizi wasaidizi kufanya zoezi la uchaguzi vizuri kwakuwa wameaminiwa hivyo wanapaswa kufanya kazi vizuri ili wasimwangushe aliyewaamini kulitekeleza jukumu hilo.
Naye Josephat Bubegwa mratibu wa uchaguzi ngazi ya jimbo amesema wasimamizi wasaidizi wote wanapswa kuwajibika kwa kufuata taratbu za utumishi wa umma na kwamba watawajibishwa kulingana na matendo yao katika wakati wote wa zoezi la uchaguzi.
Wasimazi wa Uchaguzi wakiapishwa
Akizungumza Jabil Timbako, mratibu wa uchaguzi eneo la uhamsishaji wa umma amesema wanaendelea kuihamasisha jamii kushiriki kikamilifu katika kujiandikisha katika daftari na kwamba wanaelewa muenendo mzima wa zoezi.
Amesema wanafanya pia uhamasihaji kwa makundi maalum ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kushiriki katika zoezi hilo kikamilifu