WANANCHI WATAKIWA KUACHA IMANI POTOFU KUHUSU CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI
Posted on: April 19th, 2024Akifungua kikao cha afya ya msingi Mkuu wa wilaya ya kigoma Salum Kalli amesema kampeni ya kitaifa ya utoaji wa chanjo dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi HPV Kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi miaka 14 , chanjo hii inatajiwa kuanza kutolea kuanzia tarehe 22 April 2024 hadi tarehe 28 April 2024. Ambapo wilaya ya kigoma inatajiwa kuchanja Zaidi ya wasichana 42,414 ambapo wasichana 20,604 kwa upande wa manispaa ya kigoma na wasichana 21,810 halmashauri ya kigoma.
wajumbe wakiwa wamesimama kumkaribisha mkuu wa wilaya ya kigoma salum kalli kwenye kikao cha chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri kuanzia miaka 9 hadi 14
Amesema kalli lengo la serikali ni kuwapa chango wasichana wote wenye umri wa miaka 9 hadi miaka 14 na chanjo hii nisalama na inatolewa bure bila malipo, wapo watu wamekuwa wakiwatisha watu na kuwambia chanjo hii si salama hii imethitishwa na wataalamu kuwa chanjo hii ni Bora na ni salama Kwa watoto wetu kama ilivyo kwa chanjo zingine.
Zoezi hili litafanywa na watoa huduma za afya Kwa kushirikia na walimu, watakwimu katika vituo vya kutolea huduma mashuleni na kwenye jamii, watoto wengi wenye umri huu wanapatika shule za msingi,shule za sekondari, viuoni tuhakikishe tunawafikia wote katika maeneo yote ili kufika malengo ya kuchanja Zaidi ya wasichana 42,414.
Mkuu Kalli pia ametumia nafasi hiyo kuwaombea viongozi wa dini zote wawasitize waumini na kuwa hamasisha wananchi katika nyumba zao za ibada kushiriki kikamilifu katika Zoezi hili la chanjo kwa wasichana wote wenye umri wa miaka 9 hadi 14
wajumbe wakisikiliza hoja za kikao cha chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi
Naye Kaimu mganga Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya kigoma Aswile Mwambembe amesema tunatoa kinga zidi ya kirusi anayeitwa Huma. Papilloma Virus ambaye ana sababisha saratani mbalimbali ikiwe saratani ya mlango wa kizazi, saratani hii ndio inaongoza kusababisha vifo vya wanawake wengi Zaidi niwahakikishie kuwa chanjo hii ni salama na tayari imefanyiwa majaribio mkoani Kilimanjaro, walengwa ni wasichana waliozaliwa mwaka 2010 ha mwaka 2015
wajumbe wakisikiliza hoja za kikao cha chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi
Chanjo hii inatolewa bure kwa njia ya sindano kwenye msuli wa mkono wa kushoto ambapo mlengwa anatakiwa kupewa dozi moja pekee kwa wasichana wasio na maambukizi ya virusi vya ukimwi na wasichana walio na virus vya ukimwi utaratibu wa kawaida utaendelea wa kupewa dozi katika vipindi vitatu.