WAKULIMA I500 KIGOMA DC WAFIKIWA NA ELIMU YA SHAMBA DARASA

Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwa kushirikiana na Shirika la Chakula Duniani (FAO)imepeleka Elimu ya shamba Darasa kwa wakulima zaidi ya 1500 itakayowawezesha kutekeleza shughuli za kilimo kuendana na mabadiliko ya tabianchi na kuongeza tija.
Hayo yamesemwa leo tarehe 12 Juni,2025 na Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bw.Ramadhan Mpasiwakomu baada ya kukabidhi Baiskeli 20 kwa Viongozi wa Wakulima katika 5 za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Bw.Mpasiwakomu ametaja Kata zilizofikiwa chini ya Mradi wa Pamoja wa Kigoma kuwa ni Kata za Simbo,Mungonya,Bitale,Kalinzi na Nyarubanda ambapo kupitia Viongozi wa Wakulima Elimu ya Shamba Darasa imeendelea kupelekwa ili kuwawezesha Wakulima kufanya kilimo cha tija.
Ameongeza kuwa Baiskeli 20 walizokabidhiwa Viongozi wa Wakulima ni ufadhili wa Serikali ya Norway ili kufikia vijiji na vitongoji kwa urahisi na kusambaza elimu ya ugani kwa wakulima,wakati huu ambapo Serikali inatekeleza mpango wa Kilimo awamu ya pili ambao unategemea wadau.
"Juhudi ambazo Shirika la Chakula Duniani imefanya kwa Halmashauri yetu itawezesha kuwepo kwa Usalama wa chakula,Lishe ya kutosha na kupunguza udumavu". amesisitiza Bw.Mpasiwakomu.
Kwa upande wao baadhi ya Viongozi wa Wakulima wamesema Baiskeli walizopewa zitaongeza Kasi ya utendaji kazi na kutatua changamoto ya kuwafikia wakulima kwa wakati kwenye usambazaji wa elimu ya ugani hususan kwenye maeneo yasiyofikika kwa urahisi.
@ortamisemi
@kigomars
@maelezonews
@msemajimkuuwaserikali
@official_taritanzania
@ikulu_mawasiliano
@samia_suluhu_hassan