TIMU YA WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA IMEKAGUA MRADI WA KIMKAKATI WA SOKO LA KIMATAIFA LA KAGUNGA.
Posted on: July 18th, 2020Timu ya wakuu wa idara na vitengo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma imetembelea na kukagua mradi wa kimkakati wa soko la kimataifa ya Kagunga. Soko hilo linajengwa na kampuni ya kizalendo ya Bogeta Engineering LTD ya jijini Dar es Salaam kwa gharama ya zaidi shilingi bilioni 1.49. Pindi soko hili litakapokamilika itakuwa ni chachu ya mandeleo kwa kukuza uchumi na kuongeza kipato kwa Halmashauri. Mradi huu ni miongoni mwa miradi mingi ya kimkakati inayotekelezwa na serilkali nchi nzima.