TAASISI YA MKAPA YAKABIDHI NYUMBA 30 NA BAISKELI 200 KUIMARISHA MFUMO WA AFYA KIGOMA
Posted on: March 27th, 2017
TAASISI ya Benjamini MKAPA yakabidhi Nyumba M-pya 30 za Watumishi wa Afya Mkoa wa Kigoma katika Hafla fupi iliyofanyika Zahanati ya Kalinzi Wilayani Kigoma. Nyumba hizo zilizokabidhiwa ni miongoni mwa Nyumba 480 zilizojengwa katika Halmashauri 51 Inchini kupitia Mradi wa Uimarishwaji wa Mifumo ya Afya unaofadhiliwa na Global Fund.
Mkurugenzi wa TAASISI ya Benjamini MKAPA Dr. Ellen Mkandya Senkoro akitoa Taarifa ya Ujenzi wa Nyumba hizo katika Hafla fupi iliyohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali (Mstaafu) Emmanuel Maganga kama Mgeni rasmi akiambatana na Viongozi wengine wa Mkoa na Wilaya, Dr. Ellen amesema Nyumba hizo zimegharimu kiasi cha TShs 1.8 Billion sawa na wastani wa Shs 58.8 millioni kwa kila Nyumba moja na kuongeza kuwa Nyumba hizo zimejengwa katika Vituo vya Tiba 5 vilivyopo Wilaya ya Kigoma ambapo ni wastani wa Nyumba 2 kwa kila kituo)
Aidha Dr. Ellen ameeleza kuwa TAASISI ya Benjamini MKAPA imefanya Ujenzi kama huo katika Wilaya ya Kasulu na Kibondo ambapo Nyumba 10 zenye thamani hiyo zimejengwa kwa kila Wilaya.
Sambamba na hilo TAASISI ya Benjamini MKAPA katika Hafla nyingine fupi iliyofanyika Hospitali Rufaa MAWENI, imekabidhi Vitendea Kazi vya Uimarishaji wa Huduma za Afya zikiwemo Baiskeli 200, Mabegi 225, Buti 25 na makoti ya mvua 25 vyenye Thamani ya TShs 44 million kwa uongozi wa Mkoa wa Kigoma. Msaada huo unalengo la kuwawezesha wahudumu wa afya ngazi ya jamii mkoani Kigoma kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Licha ya juhudu zinazofanywa wa serikali kwa kushirikiana wadau mbalimbali hali ya utoaji wa huduma ya afya katika Halmashauri ya wilaya ya Kigoma sio ya kuridhisha kwani mpaka sasa Halmashauri ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya vya serikali na binafsi 43, kati ya hivyo zahanati ni 39 na vituo vya afya 4, hata hivyo halmashauri ya wilaya haina Hospitali.
Idara ya afya ina mahitaji ya watumishi 556, waliopo ni 166, hivyo ina upungufu wa watumishi 390. Mahitaji ya nyumba za watumishi ni 116, zilizopo 47 na upungu ni 69.
Kwa upande wa idadi ya kaya zilizojiunga kwenye mfuko wa Jamii wa Afya ya Jamii (CHF) ni kaya 6,138 kati ya Kaya 41,934 zilizopo.
Aidha hali ya usafirishwaji kwa wagonjwa bado ni changamoto kwani mpaka sasa idara ina maboti 2 lakini yote ni mabovu pia Idara afya ina magari 2 ya kubebea wagonjwa kati ya hayo 1 tu ndio linalofanya kazi. Magonjwa yanayoongoza katika Halmashauri ni maambukizo ya mfumo wa upumuaji (ARI) kwa 27.7%, Minyoo ya tumbo 18%, Malaria 14%, Kuharisha 9.6% na homa za mapafu (Pneumonia) 11.1%.
NA. SHABAN AKAPELA
Habari na. Shaban Akapela (Afisa Habari KDC) anapatikana 0763112532 Email : juniorkapera@gmail.com