SERIKALI,THPS YAJA NA MABORESHO UPIMAJI UKIMWI HOMA YA INI NA KASWENDE

Serikali kwa kushirikiana na shirika la Tanzania Health Promotion Support(THPS) imedhamiria kukabiliana na Maambukizi ya magonjwa ya UKIMWI,Homa ya Ini pamoja na Kaswende kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto kwa kuwajengea uwezo watumishi kuhusu maboresho ya kisayansi kwenye upimaji wa magonjwa hayo.
Mafunzo hayo yatakayofanyika kwa siku 2 yameanza leo tarehe 16 hadi 17 Julai,2025 kwa watumishi wa afya 37 wanaotoa huduma katika kliniki za afya ya uzazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma yaliyoratibiwa na ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.