• Webmail
  • Maswali ya Mara kwa mara
  • Wasiliana nasi
Kigoma District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali watu
    • Planning and Management
    • Finance and Accounts
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Procurement and Supply
    • Economy and Production
    • Miundombinu
    • Local Government
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Guidelines
    • Procedures
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Media Center
    • Habari
    • Matangazo kwa umma
    • Maktaba
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Videos

SERIKALI KUJENGA ZAHANATI KIJIJI CHA KILEMBA

Posted on: May 7th, 2024

Mwenyekiti wa kijiji wa Kilemba kata ya Mkigo halmashauri ya wilaya ya Kigoma Issa Kihamuzi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kutoa shilingi milioni 100 kwaajili ya ujenzi wa zahanati katika kijiji chao.

Amesema kukamilika kwa zahanati hiyo kutasaidia kuondoa changamoto ya wananchi  kutibiwa katika zahanati ya Mkigo, hospitali ya Heri Miission na Nyamasovu iliyopo halmashauri ya wilaya ya Buhigwe pamoja na kituo cha afya cha Matyazo.

“Wananchi wamekuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya, kutoka Kilemba mpaka Mkigo wananchi hutembea kati ya nusu saa hadi saa moja na nusu, na inapotokea dharura ya magonjwa ya usiku au wajawazito inatubidi kukodisha gari kwa gharama kubwa kuanzia elfu 30,000-50,000”. Amesema  Kihamuzi

Mwenyekiti ameongeza kuwa changamoto zaidi ipo kwa akina mama wajawazito ambao inawabidi kutembea umbali mrefu kufuata huduma katika zahanati ya kata ya Mkigo ambapo baadhi yao hupatwa na changamoto ya kupoteza watoto au wao wenyewe kupoteza maisha na hivyo kukamilika kwa zahanati hiyo kutaokoa maisha ya mama na mtoto.

Hata hivyo Mwenyekiti amesema kukamilika kwa zahanati hiyo ya kutarahisisha huduma za afya kwa wananchi wa kata za jirani na nchi jirani ya Burundi, vilevile itasaidia kupunguza gharama za usafiri ambazo wananchi wamekuwa wakizipata.


Mwenyekiti Kihamuzi amemuomba Rais mara zahanati hiyo itakapokamilika wapelekewe vifaa vyote muhimu pamoja na wafanyakazi ili kuboresha huduma hizo.

Naye  Eliasia Mayani mhudumu wa wa afya ngazi ya jamii, amefurahishwa na hatua ya serikali ya kuwajengea zahanati kwakuwa watapungunguza changamoto ya ushawishi kwa kina mama wajawazito kuanza huduma za kliniki mapema i kwakuwa watapata kwa kijiji mwao pa bila kutembea umbali mrefu.

Naye Nyamang’elele Mtaki afisa mifugo kata ya Mkigo, amesema hakukuwa na utulivu wa wafanyakazi kutokana na kukosekana kwa huduma za afya, anaamini zahanati hiyo itakapokamilika itakuwa chachu kwa watumishi kutulia katika vituo vyao vya kazi.

Latest Announcements

  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA

    read more
  • TANGAZO LA AJIRA

    read more
  • TANGAZO LA MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA

    read more
  • TANGAZO LA KAZI YA MUDA

    read more
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA VIJANA, WANAWAKE NA WATU WENYE ULEMAVU

    read more
  • View More

Habari M-pya

  • WAKULIMA WA ZAO LA MCHIKICHI WATAKIWA KUTUMIA MBEGU BORA ILI KUONGEZA UZALISHAJI NA KUKUZA KIPATO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA YAPIGA HATUA UTOAJI WA CHAKULA SHULENI
  • SERIKALI YAOKOA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 60 KWENYE UJENZI WA MADARAJA YA MAWE KOTE NCHINI
  • DC.DKT. CHUACHUA ASISITIZA WAZAZI KUWAWEZESHA WANAFUNZI KUPATA CHAKULA SHULENI
  • DCC KIGOMA DC YAPITISHA MCHAKATO WA MGAWANYO WA KATA
  • More

Wasiliana nasi

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
THE DISTRICT EXECUTIVE DIRECTOR
Postal Address: P.O.Box 332, KIGOMA
Telephone: 028 2804865
Barua pepe: ded@kigomadc.go.tz
Mobile: 028 2804865
P.O.Box 332 KIGOMA
Postal Address: MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA KIGOMA
Telephone: 028 280 271 9
Barua pepe: ded@kigomadc.go.tz
Mobile: +255752337486

Tovuti zinazo fanana

  • Kigoma Ujiji Mc
  • Halmashauri ya Wilaya Uvinza
  • Halmashauri ya Wilaya Buhigwe
  • Halmashauri ya Wilaya Kasulu
  • Halmashauri ya Mji wa Kasulu
  • Halmashauri ya wilaya Kibondo
  • Halmashauri ya wilaya Kakonko

Tovuti Zinazo husiana

  • OFISI YA RAIS TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI (NECTA)
  • WIZARA YA UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  • MKOA WA KIGOMA
  • TOVUTI YA TAIFA
  • MFUMO WA MADENI YA WATUMISHI SERIKALINI
  • SALARY SLIP PORTAL

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2024GWF . All rights reserved.

  • Vigezo
  • Sera za Usiri
  • Maswali ya Mara kwa mara
  • Ramani