SERIKALI IMETEKELEZA UJENZI WA NYUMBA YA WALIMU (2 IN 1) KATIKA SHULE YA SEKONDARI NKUNGWE

Serikali imetekeleza ujenzi wa nyumba ya Walimu(2 in1 ) katika Shule ya Sekondari ya Nkungwe katika Kata ya Nkungwe kwa thamani ya shilingi milioni 110.
Kukamilika kwa ujenzi wa nyumba hii kutawawezesha walimu kuishi karibu na mazingira ya shule na kuepuka adha ya kusafiri umbali mrefu kila siku kwenda Shuleni na hivyo kutekeleza shughuli za Ufundishaji kwa ufanisi.
Utekelezaji wa mradi huu wa nyumba ya Walimu ni mwendelezo wa Mafanikio makubwa kwenye uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu unaotekelezwa na Serikali ya awamu ya 6 ndani ya kipindi cha miaka 4 ya madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma pamoja na Wanakigoma wote wanatoa shukrani zao za dhati kwa Mhe.Rais Dkt.Samia kwa Mafanikio haya makubwa na ya kupigiwa mfano ndani ya Halmashauri.
Kwa pamoja Tujenge Halmashauri yetu na Taifa letu kwa ujumla.