MKUU WA WILAYA KIGOMA AMEAGIZA SHULE ZOTE KUTOA CHAKULA
Posted on: February 9th, 2024
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Mhe. Salum Kalli ameziagiza shule zote za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kutoa Chakula shuleni, Amesema hayo, Leo tarehe 09, Februari, 2024, Akiwa kwenye kikao cha tathmini ya mkataba wa Lishe Cha Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwa robo ya Pili, Oktoba-Desemba 2023.
Mhe. Mkuu wa Wilaya Amewaagiza wakuu wa Divisheni za Elimu Msingi na Sekondari kuhakikisha wanawaagiza walimu Wakuu na Wakuu wa shule kuwaelimisha wazazi kuchangia chakula Ili wanafunzi waweze kupata chakula shuleni. Pia amewaagiza Maafisa watendaji wa Kata kutoa Elimu kwa wazazi kuhakikisha wanafunzi wanakula chakula shuleni.
Aidha Mhe. Mkuu wa wilaya amesisitiza shule zote zilizo na mashamba au maeneo ya kulima zihakikishe zinalima mashamba kama njia mbadala ya kufanikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni.
Wajumbe wa kamati ya lishe Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
Wajumbe wa kamati ya Lishe wakisikiliza hoja za kikao