MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA ATEMBELEA MIRADI YA UJENZI WA MADARASA KATIKA MPANGO WA KUPAMBANA NA UVIKO-19

Tarehe 10 Novemba 2021 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bi. Rose Robert Manumba amefanya ziara ya kutembelea miradi yote ya ujenzi wa madarasa yanayojengwa kutokana na mkopo nafuu wa kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). Mradi huu wa ujenzi wa madarasa unaotekelezwa chini ya mpango wa kupunguza kuenea kwa UVIKO 19, utapunguza msongamano kwa wanafunzi wanaotarajiwa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2022. Jumla ya madarasa 69 yanajengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma katika Kata mbalimbali. Miradi imeonekana kuanza vizuri na muendelezo ni mzuri mpaka sasa. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri amesisitiza bidii na kuwajibika ili madarasa yamalizike kwa wakati uliopangwa na yaanze kutumika mwakani kwa wanafunzi hasa kwa kidato cha kwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Rose Manumba (Wa pili kutoka kushoto), Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi ya Halmashauri Bw. Nassir Kirusha (Wa tatu kutoka kushoto) na Mtaalamu wa ujenzi kutoka Halmashauri (Wa nne kutoka kushoto) wakifualia ujenzi hatua za ujenzi wa magarasa. Wengine kwenye picha ni mafundi.
Ujenzi ukiendelea katika hatua ya kupanga Mawe kwenye msingi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Rose Manumba (Wa pili kutoka kushoto) akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa mradi