MAKAMU MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO HALMASHAULI YA KIGOMA
Posted on: January 26th, 2024Makamu mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi CCM , Ndugu Rehema Sombi Omary leo tarehe 25/01/2024, Amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya wilaya ya kigoma inayotekelezwa chini ya serikali ya awamu ya sita .Amekagua ujenzi wa chuo kikuu cha uhasibu tawi la kigoma , ujenzi wa kituo cha afya cha kisasa kata ya Simbo, madarasa manne S/M kidahwe yaliyofadhiliwa na mradi wa boost pia amekagua Mradi wa vijana wa nyama choma Kidahwe.Aidha amewapongeza viongozi wa halmashauri kwa usimamizi mzuri wa miradi na kuahidi kuwa serikali ya awamu ya sita ya Rais SAMIA SULUHU HASSAN kuwa imejipanga kuleta miradi zaidi ya hii hivyo amewataka wananchi wajiandae kuipokea na kuitunza miradi hiyo.
Majengo ya chuo kikuu cha uhasibu tawi la kigoma
Majengo ya kituo cha Afya Simbo