• Webmail
  • Maswali ya Mara kwa mara
  • Wasiliana nasi
Kigoma District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali watu
    • Planning and Management
    • Finance and Accounts
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Procurement and Supply
    • Economy and Production
    • Miundombinu
    • Local Government
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Guidelines
    • Procedures
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Media Center
    • Habari
    • Matangazo kwa umma
    • Maktaba
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Videos

PROGRAM YA SHULE BORA YAFANYA MAFUNZO YA USHIRIKIANO WA WAZAZI NA WALIMU (UWaWa)

Posted on: February 28th, 2023

Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kupitia Programu ya Shule Bora imeendesha mafunzo yanayohusu Ushirikiano wa Wazazi na Walimu katika (UWaWa). Mafunzo haya yanalenga kujengeana uwezo kati ya wazazi na walimu ili kuendela kushirikiana katika maendeleo ya Shule na Elimu kiujumla. 

Pichani juu: Washiriki wa Mafunzo wakiendelea na Mafunzo.


Shule Bora ni Programu ya Serikali chini ya ufadhili wa shirika la UK aid, Ni Programu inayolenga kuboresha ubora wa elimu katika ngazi ya awali na msingi na kuleta usawa wa elimu kwa wasichana, wavulana na watoto wenye mahitaji maalumu na pia kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji. Programu hii inaendeshwa katika Mikoa 9 ya Tanzania Bara, Mkoa wa Kigoma ukiwa miongoni mwa mikoa hiyo 9.

Pichani juu: Washiriki wakifanya majadiliano wakati wa Mafunzo.


Mafunzo haya ya Ushirikiano wa Wazazi na Walimu (UWaWa) yanafanyika katika Shule ya Msingi Nkema iliyopo Kata ya Mwandiga kuanzia tarehe 28 Februari, 2023 hadi tarehe 02 Februari, 2023 kwa kundi la kwanza. Walengwa kutoka Kata 16 za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wanashishiriki. Walengwa wa Mafunzo hayo ni Walimu Wakuu wa shule za msingi, Wenyeviti wa Kamati za shule na Maafisa elimu wa Kata.

Pichani juu: Washiriki wa Mafunzo wakifanya majadiliano juu ya mada husika.


Katika mafunzo haya dhana ya shule kuwa mali ya jamii imeendela kusistizwa ili jamii iweze kushiriki vizuri zaidi katika maendeleo ya shule. Akifungua mafunzo hayo Afisa Elimu Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Mwl. Kassim Mtili amesema ushirikiano wa wazazi na walimu ndiyo nguzo kuu ya maendela ya shule zetu ambayo itaboresha elimu. Afisa elimu amesisitiza kuwa kila mshiriki kwa nafasi yake awe sehemu ya kujenga mahusiano bora kati ya shule na wazazi. Mwalimu mkuu kama msimamizi wa sera ya elimu kwenye kituo, Afisa elimu Kata kama msimamizi wa sera ya elimu kwenye kata na wazazi kama sehemu ya jamii shule husika.

Pichani juu: Afisa Elimu wa Awali na Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Mwl. Kassim Mtili (Katikati mwenye Koti) akifungua mafunzo hayo tarehe 28 Februari, 2023.


Mafunzo haya yanafanyika wakati ambao wazazi wamekuwa ni sehemu muhimu sana kuiwezesha serikali kuendelea kutekeleza mipango ya kuboresha elimu nchini huku dhana ya ushirikishwaji wa wananchi ikisisitizwa ili kufikia mafanikio katika sekta ya elimu.

Washiriki zaidi ya 230 kutoka Kata 16 ambao ni Wenyeviti wa Kamati za Shule, Walimu Wakuu na Maafisa Elimu Kata wanapewa mafunzo haya ya Ushirikiano wa Walimu na Wazazi ili baada ya mafunzo hayo waende wakaimarishe Ushirikiano katika usimaamizi wa shule.

Pichani juu: Washiriki wakimsikiliza mshiriki mwenzao wakati wa majadiliano. 


Pichani juu: Washiriki wa Mafunzo wakiendelea na Mafunzo.


Pichani juu na chini: Washiriki wa Mafunzo wakiendelea na Mafunzo.

Latest Announcements

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MUDA

    read more
  • WRITTEN INTERVIEW RESULTS MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA PILI

    read more
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA VIJANA, WANAWAKE NA WATU WENYE ULEMAVU

    read more
  • View More

Habari M-pya

  • WALENGWA WA KAYA MASKINI WAHIMIZWA KUENDELEZA UJUZI NA MIRADI WALIYOANZISHA
  • JESHI LA MAGEREZA KWITANGA LAFANYA USAFI HOSPITALI YA WILAYA YA KIGOMA LIKIFANYA MAADHIMISHO YA WIKI YAKE
  • SERIKALI YAKABIDHI MABOTI MAWILI YENYE THAMANI YA TSH MILIONI 100 KWA AJILI YA KUIMARISHA DORIA ZIWA TANGANYIKA
  • NG’OMBE 7,000 KUCHANJWA DHIDI YA HOMA YA MAPAFU KIGOMA DC
  • CHMT KIGOMA DC YAFUATILIA KWA UKARIBU HUDUMA ZA AFYA MWAMBAO WA ZIWA TANGANYIKA
  • More

Wasiliana nasi

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
THE DISTRICT EXECUTIVE DIRECTOR
Postal Address: P.O.Box 332, KIGOMA
Telephone: 028 2804865
Barua pepe: ded@kigomadc.go.tz
Mobile: 028 2804865
P.O.Box 332 KIGOMA
Postal Address: MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA KIGOMA
Telephone: 028 280 271 9
Barua pepe: ded@kigomadc.go.tz
Mobile: +255752337486

Tovuti zinazo fanana

  • Kigoma Ujiji Mc
  • Halmashauri ya Wilaya Uvinza
  • Halmashauri ya Wilaya Buhigwe
  • Halmashauri ya Wilaya Kasulu
  • Halmashauri ya Mji wa Kasulu
  • Halmashauri ya wilaya Kibondo
  • Halmashauri ya wilaya Kakonko

Tovuti Zinazo husiana

  • OFISI YA RAIS TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI (NECTA)
  • WIZARA YA UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  • MKOA WA KIGOMA
  • TOVUTI YA TAIFA
  • MFUMO WA MADENI YA WATUMISHI SERIKALINI
  • SALARY SLIP PORTAL

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2024GWF . All rights reserved.

  • Vigezo
  • Sera za Usiri
  • Maswali ya Mara kwa mara
  • Ramani