MAAFISA WATENDAJI WA KATA 16 ZA HALMASHAURI YA KIGOMA WAMPONGEZA MKURUGENZI KWA KUSHUGHULIKIA MADAI YA STAHIKI ZAO
Posted on: April 2nd, 2024Watendaji 16 wa kata za halmashauri ya wilaya ya Kigoma wamempongeza mkurugenzi wa halmashauri hiyo Chiriku Chilumba kwa kumpatia mbuzi kutokana na kuhakikisha kuwa stahiki zao zimelipwa kwa wakati.
Akiongea mwenyekiti wa watendaji hao, Lulinda Rashid kutoka kata ya Ziwani amesema wanafurahishwa na utendaji kazi wake,na kama mwajiri aendelee kufanya kazi vizuri na kutetea haki za watumishi kama mwajiri.
Mkurugenzi akiwashukuru watendaji kwa zawadi ya beberu waliyompa
“Amefika kwenye halmashauri ya Kigoma hivi karibuni, ndani ya muda mfupi aliokaa tumelipwa stahiki zetu tulizokuwa tunadai, ni kiongozi mzuri” Amesema Rashid.
Akipokea shukrani hizo, mkurugenzi Chilumba amesema pongezi hizo ni ishara ya kuboresha utendaji kazi na usimamizi mzuri wa majukumu.
Amesema shukrani hizo si zake peke yake, Bali ni kwaajili ya wakuu wote wa idara na wafanyakazi wa halmashauri hiyo kwani wanafanya kazi kwa ushirikiano.
“Mafanikio haya yanategemeana na mtazamo wangu lakini ushirikiano na watumishi wengine wakiwemo wakuu wa idara,tuliahidi kushirikiana kuhakikisha pale penye changamoto tunaziondoa na tumefanikiwa” Amesema Chilumba.
Mkurugenzi Chilumba amewashukuru watendaji hao na kushukuru jitihada zinatokana na ushirikiano anaupata kutoka kwa wakuu wa idara pamoja na wengine kwani anaamini katika jitihada za kila mmoja katika kufikisha lengo na kusema kuwa bado upo mipango mizuri ya kuhakikisha kwamba changamoto zilizopo zinapunguzwa na hakikishe kuwa zinakwisha.
Picha ya pamoja ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kigoma akiwa na watendaji wa kata 16 za halmashauri hiyo