MAAFISA UGANI MKOANI KIGOMA WAPATIWA VITENDEA KAZI
Posted on: August 16th, 2024
Maafisa ugani mkoani Kigoma wametakiwa kujitathmini katika utendaji kazi wao, kwa kupima matokeo ya uzalishaji katika sekta ya kilimo kabla na baada ya kupokea vitendea kazi vilivyotolewa na serikali kwaajili ya kuboresha sekta ya kilimo mkoani humo.
Akizungumza Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, katika hafla ya kukabidhi vitendeaa kazi kwa maafisa ugani, Hassan Rugwa amesema ni muhimu kufanya tathimini ili kupata matokeo ya thamani inayoongezeka katika uzalishaji wao ili kuleta tija na ufanisi katika sekta hiyo kutokana na vifaa vinayotolewa na maafisa ugani wanaojiriwa.
Baadhi ya wakurugenzi wa Mkoa wa kigoma wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma
“Mpaka sasa mkoa umepokea pikikipi 134, vifaa vya kupima udongo, vishikwambi 440, mavazi rasmi ya kazi 175, na vifaa vingine vingi, tunataka kuona hivi vitendea kazi vikileta matokeo chanya katika uzalishai, ,tufanye tathmini ya kazi zetu ili vitendea kazi tunavyoendelea kupokea vinaendana na matokeo, tuhakikisha tunaongeza uzalishaji kabla na bada ya kupkea vifaa” amesema Rugwa.
Awali akizungumza Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji mkoani humo, James Peter amesema serikali imetoa magwanda kazi 175, pamoja na magari mawili yaliyotolewa katika halmaashauri ya wilyaya ya Buhigwe pamoja na ofisi ya mkoa kwaajili ya ufuatiliaji na kuongeza usimamizi kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji na kutimiza ndoto ya serikali ya kuboresha sekta ya kilimo.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kigoma,Thobias Andengenye amewataka maafisa hao kutojitofautisha wao na vitendea kazi vinavyotolewa ili waweze kuvitunza kwa uchungu na kuleta ufanisi katika shughuli zao kwani kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya vitendea kazi vinavyotolewa kwa wafanyakazi ambapo wamekuwa wakivitelekeza hata pale vinapohitaji marekebishi madogo wakisubiri serikali ifanye.