KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI TAREHE 10 FEBRUARI, 2022
Posted on: February 10th, 2022Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kimeketi leo tarehe 10 Februari, 2022 na ajenda mbalimbali zimepitiwa na waheshimiwa Madiwani. Miongoni mwa ajenda hizo ni taarifa za kamati za Madiwani ambazo zimejadiliwa na kupokelewa na Baraza la Madiwani. Pia miongoni mwa mambo yaliyoongelewa ni pamoja na ujenzi wa ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kigoma, ujenzi wa kituo cha afya Kagunga, ubunifu kukusanya mapato na uwekezaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma n.k. Baraza limehudhuriwa na wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma pamoja na wageni mbalimbali walioalikwa akiwemo kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigoma (DAS), Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kigoma na taasisi na vyombo mbalimbali vya usalama.
Pichani juu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bi. Rose Robert Manumba (Aliyesimama) akisema jambo katika Baraza hilo la Madiwani.
Diwani wa Kata ya Kalinzi Mh. Ignas R. Helanya akichangia hoja katika Baraza la Madiwani lililofanyika tarehe 10 Februari, 2022 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Kaimu Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ndg. George Daniel Onyango (Aliyesimama) akitoa mwongozo katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika tarehe 10 Februari, 2022.
Daktari Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Daktari Lusajo Mwakajoka (Aliyesimama) akitoa ufafanuzi katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika tarehe 10 Februari, 2022.
Afisa Rasilimali Watu wa Halmashuri ya Wilaya ya Kigoma Bw. Bennet Ninalwo akifafanua jambo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri wa Wilaya ya Kigoma tarehe 10 Februari, 2022.