KAMATI YA SIASA YA CCM (W) KIGOMA YARIDHISHWA UTEKELEZAJI WA MIRADI KIGOMA D.C

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kigoma Mhe.Almesh Mayonga amesema ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu na afya kwa kuzingatia Ilani ya CCM kwenye maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Mhe.Mayonga amesema hayo leo tarehe 23 Juni,2025 wakati kamati ya Siasa ya CCM Kigoma ilipotembelea na kukagua utekelezaji wa Mradi wa Hospitali ya Wilaya ya Kigoma iliyoko Mahembe,na ujenzi wa Bwalo la Wanafunzi katika shule ya Sekondari ya Mwandiga.
Mhe.Mayonga akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mhe.Dkt.Rashid Chuachua,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Mwl.Chiriku Hamisi Chilumba pamoja na wataalam wametembelea Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kigoma unatekelezwa kwa awamu ambapo Serikali ilitenga kiasi cha Shilingi Bil.3 kwaajili ya Ujenzi wa majengo mbalimbali pamoja na ununuzi wa Vifaa tiba,hatua itakayowawezesha Wananchi kupata huduma karibu na makazi yao.
Mwenyekiti wa CCM Mhe.Mayonga pamoja na kumpongeza Mhe.Mkuu wa Wilaya ya Kigoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma amesema lengo lao ni kuona Ilani ya CCM inatekelezwa kikamilifu kwa kuhakikisha Miradi yote ambayo Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameleta fedha inatekelezwa kwa maslahi ya Wananchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mhe.Dkt Rashid Chuachua amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha Miradi ya maendeleo iliyopo kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo ya Elimu,Afya,Maji na Miundombinu inakamilika kwa wakati huku akisisitiza wananchi kuendelea kuwa na imani na Serikali kwa kuwa ina dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo.