D.C DKT.CHUACHUA,KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WAKAGUA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mhe.Dkt.Rashid Chuachua ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma hapo baadae mwezi Septemba.
Dkt.Chuachua akiwa ameongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya pamoja na Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wamekagua mradi wa Kituo kipya cha Afya cha Mwandiga,majengo ya Darasa na vyoo katika Shule ya Msingi Ukombozi iliyopo Kata ya Mkongoro,mradi wa vijana wa 'Motomoto Furniture' uliopo Kata ya Mungonya pamoja na mradi wa Tanki la Maji katika Kata ya Mkigo.