• Webmail
  • Maswali ya Mara kwa mara
  • Wasiliana nasi
Kigoma District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Rasilimali watu
    • Planning and Management
    • Finance and Accounts
    • Ukaguzi wa Ndani
    • Procurement and Supply
    • Economy and Production
    • Miundombinu
    • Local Government
    • Ustawi wa Jamii
    • TEHAMA
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Guidelines
    • Procedures
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Media Center
    • Habari
    • Matangazo kwa umma
    • Maktaba
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Videos

DAS NZOTA APIGA MARUFUKU MASOKO YA USIKU KWA WATOTO WA UMRI WA CHINI YA MIAKA 18

Posted on: June 17th, 2025

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigoma Mhe.Mganwa Nzota amewapiga marufuku Wazazi wanaowatuma watoto wao walio chini ya umri wa miaka 18 kufanya Biashara kwenye masoko ya usiku ili kuwaepushia  vitendo vya ukatili wa kijinsia.


DAS Nzota ametoa mwito huo leo tarehe 16 Juni,2025 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Kagina katika Kata ya Kagongo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.



"Tambueni watoto wote wanaohusishwa kwenye masoko ya usiku ili Wazazi wao tuweze kuwachukulia hatua za kisheria,tukibaini mtoto yuko sokoni usiku katika wakati ambao anatakiwa ajisomee,mchukueni mtoto huyo mpaka nyumbani kwao na Wazazi wake tumchukulie hatua za kisheria"amehimiza DAS Nzota


Amesema tukiweza kudhibiti jambo hilo watoto wataweza kupata muda mzuri wa kujisomea na kupunguza wigo wa vitendo hatarishi ambavyo mtoto anaweza kukutana navyo katika mazingira ya masoko ya usiku yanayodumu hadi muda wa usiku mkubwa.


Aidha DAS Nzota amewasisitiza wazazi kutenga muda wa kutosha wa kuwasikiliza watoto wao na kusikiliza changamoto wanazozipitia ili kupunguza matendo ya Ukatili wa kijinsia kwa watoto kwa kuwalinda watoto huku akihimiza kuwa jukumu la kwalinda watoto ni jukumu la jamii nzima.


Amesema jitihada zinazofanywa na Serikali za kuboresha huduma za Afya na Elimu zinapaswa kuungwa mkono na Mzazi mmoja mmoja kwa kuchangia michango itakayowawezesha watoto kupata huduma za msingi ili waweze kufikia ndoto zao siku za usoni.


Chimbuko la Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika hutokana na mauaji ya watoto zaidi ya Elfu 2 yaliyofanywa na utawala wa Makaburu katika Kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini tarehe 16 Juni,1976 ambapo kwa mwaka huu Maadhimisho hayo yamebeba Kaulimbiu isemayo "Haki za Mtoto,tulikotoka,tulipo na tunakoenda'

Latest Announcements

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MUDA

    read more
  • WRITTEN INTERVIEW RESULTS MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA PILI

    read more
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA VIJANA, WANAWAKE NA WATU WENYE ULEMAVU

    read more
  • View More

Habari M-pya

  • WALENGWA WA KAYA MASKINI WAHIMIZWA KUENDELEZA UJUZI NA MIRADI WALIYOANZISHA
  • JESHI LA MAGEREZA KWITANGA LAFANYA USAFI HOSPITALI YA WILAYA YA KIGOMA LIKIFANYA MAADHIMISHO YA WIKI YAKE
  • SERIKALI YAKABIDHI MABOTI MAWILI YENYE THAMANI YA TSH MILIONI 100 KWA AJILI YA KUIMARISHA DORIA ZIWA TANGANYIKA
  • NG’OMBE 7,000 KUCHANJWA DHIDI YA HOMA YA MAPAFU KIGOMA DC
  • CHMT KIGOMA DC YAFUATILIA KWA UKARIBU HUDUMA ZA AFYA MWAMBAO WA ZIWA TANGANYIKA
  • More

Wasiliana nasi

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
THE DISTRICT EXECUTIVE DIRECTOR
Postal Address: P.O.Box 332, KIGOMA
Telephone: 028 2804865
Barua pepe: ded@kigomadc.go.tz
Mobile: 028 2804865
P.O.Box 332 KIGOMA
Postal Address: MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA KIGOMA
Telephone: 028 280 271 9
Barua pepe: ded@kigomadc.go.tz
Mobile: +255752337486

Tovuti zinazo fanana

  • Kigoma Ujiji Mc
  • Halmashauri ya Wilaya Uvinza
  • Halmashauri ya Wilaya Buhigwe
  • Halmashauri ya Wilaya Kasulu
  • Halmashauri ya Mji wa Kasulu
  • Halmashauri ya wilaya Kibondo
  • Halmashauri ya wilaya Kakonko

Tovuti Zinazo husiana

  • OFISI YA RAIS TAMISEMI
  • BARAZA LA MITIHANI (NECTA)
  • WIZARA YA UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  • MKOA WA KIGOMA
  • TOVUTI YA TAIFA
  • MFUMO WA MADENI YA WATUMISHI SERIKALINI
  • SALARY SLIP PORTAL

Mitandao ya Kijamii

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2024GWF . All rights reserved.

  • Vigezo
  • Sera za Usiri
  • Maswali ya Mara kwa mara
  • Ramani